The Great MC and Stand up Comedian; Man of Smiles.....Natural Stress Healer......Man of Quality and Standards!! THE SERIOUS GUY ON LAUGHING AGAIN CONCERTS SERIES The pioneering founder and the King of Christian Stand Up Comedy in Tanzania!!! www.kingchavala.blogspot.com +255 713 883 797 lacs.project@gmail.com
Facebook Badge
Thursday, July 23, 2015
KIMINI CHA MTOTO WA ASKOFU-Sehemu ya 1
UTANGULIZI;
Habari ndugu
msomaji, ninaamini uko sawa na unayo afya ya mwili na akili. Kwa kuishi kwangu,
japo kwa miaka hii michache ya ujana, kwa kuzunguka kwangu huku na kule, ndani
na nje ya nchi na kwa kufanya kazi mbalimbali za ushauri wa biashara,
kufundisha vijana, kufanya ucheshi wa kujitegemea (Stand Up Comedy),
Ushereheshaji pamoja na Utafiti wa uwekezaji, nimekutana na kukumbana na mambo
mengi sana ya kufurahisha na kuogofya, ya faida nay a kuyasikitikia,lakini kwa
vyovyote vile yalivyo, yanafaa kwa fundisho na maonyo kwa jamii ya leo. Ndio
maana mimi ninajiona nina wajibu wa ktumia vipaji vyangu, waledi na kalamu
yangu kukushirikisha wewe yale yafaayo kukushirikisha ili kabla hujapatwa na
lolote uwe umejifunza na kuonywa na wale yaliowakuta.
KIMINI CHA
MTOTO WA ASKOFU ni simulizi halisi, ya mambo yaliyotokea katika maisha na
simulizi inakusanya matukio halisi ama yanayosimamia ama kujengwa katika
uhalisia. Hakuna hata tukio moja linalomlenga mtu moja kwa moja na wala hakuna
Askofu ambaye binti yake ndio anatajwa humu. Ikitokea kuna sehemu ya simulizi
hii inaonyesha kugusa au kuwiana na habari ya kweli ya mtu yeyote, basi
ichukuliwe kama mfanano tu ama mgongano tu wa simulizi hii na matukio halisi!
Mimi Fredy
Erasto Chavala ndio nimezungukwa na kukutana na haya katika simulizi hii,
Nimegharimika, nimeumia na kujikuta katika maswaibu mengi na msingi wa haya
yote ni kimini cha mtoto wa askofu, fuatana name sasa…..
Sehemu ya
1;
Nilitua
uwanja wa ndege saa mbili na nusu ya usiku badala ya saa moja na dakika kumi,
nah ii ilisababishwa na hali ya hewa kuwa mbaya na hivyo kulazimika kwenda
kutua uwanja mwingine wa jirani kabla kurejea tena pale ambapo safari yetu
ilikuwa inakusudiwa. Kutoka uwanja wa ndege mpaka mjini pana umbali kiasi, na
hivyo ilinibidi aitha nichukue tax, bajaji au pikipiki, ama nitembee sana mpaka
nje na kusubiri vibasi vidogo maarufu kama daladala, Lakini kwa bahati nzuri
kuna mama mmoja aliyekuwa na watoto wawili na mizigo ambaye nilimsaidia wakati tunapanda
ndege, na pia nikajikuta ninamsaidia tena wakati wa kushuka, huyu mama alikuja
kuchukuliwa na mwenyeji wake na hivyo nikajipata kwenye lift ya gari hilo.
Siku hiyo
ilianza kwa maluwe luwe maana dereva aliyekuwa ametumwa na mwenyeji wa yule
mama, nadhani alikuwa amelewa ama alikuwa hajafudhu kukaa barabara kubwa, maana
kilometa tatu kutoka uwanja wa ndege, alikuwa anataka kumtangulia mtu mbele na
kukata kona kulia, kitendo hicho alikifanya kwa uzembe sana kiasi cha
kumkwangua aliyekuwa mbele yake na ile kutaka kukata kona haraka mbele ya yule
aliyemkwangua, tulijukuta tunagongwa ubavuni, mlango wa nyuma, tena sehemu ya
mataa na hivyo kusababisha msongamano mkubwa sana wa magari. Gari tuliokuwa
ilikuwa ndogo aina ya Verosa na ile iliyotugonga ilikuwa Toyota prado na humo
alishuka dada mmoja ndani ya Viatu virefu na kimini cha bluu pamoja na blauzi
iyoacha maziwa yake nje kidogo na miwani ya jua ikiwa hapo katikati ya mfereji
inabembea, nwyele nyingi za kusukia na umbile matata sana. Alishuka kwa jazba
na akaanza kutukana hapo kwa mdomo nay ale matusi ya mikono. Dereva wetu
alikuwa akitetemeka sana na hivyo alikuwa hajibu kitu na mimi sikutoka nje
haraka maana kesi ile ilikuwa hainihusu sana kama mgeni, lakini baada ya muda
niliamua kutoka na kujaribu kuleta mwafaka kwa mabishano yale, basi nilipotoka
na kuuliza tatizo ni nini hata jambo hili lisimalizike, ndipo yule dada
alinigeukia kwa hasira sana, ninaamini alitaka kutamka tusi, lakini kwa bahati
tu kugeuka kwake kuligongana na sauti moja nzito iliyotoka kwenye gari nyingine
iliyokuwa inapita ikisema “Hey Rosemery Hujambo? Umepatwa na nini?” Basi
aligeuka na kuwa mpole ghafla na nikamsikia akisema “Sijambo Mchungaji,
Shikamoo! Bwana asifiwe?” Basi yule baba kama bahati tu tukagongana macho na
japo sikumfahamu kwa haraka ila alinisalimia “King Chavala ni wewe? Au
nimekufananisha?” Ni mimi mkuu! “Oh basi sawa, ninaamini jambo hilo litaisha
vema, ninaamini katika hekima zako, kadi yangu hii hapa, Ninaomba tuwasiliane
tafadhali!” Basi nikapokea ile kadi na kumuuaga na niliporudi kwenye tukio yule
dada aliamua kuchukua namba za simu za yule mama, maana aliomba kulipa gharama
za matengenezo, na basi yule dada akanitazama na ni kama alitamani kunisemesha
jambo ila alijawa na aibu, maana alishajionyesha kama mshari na mkorofi na hapo
ikajulikana kuwa ni binti wa kanisani. Aliamua kuondoka akiwa anajiuliza hivi
mimi ni nani hasa niliyeshuhudia udhihirisho wa tabia yake ya kweli. Na mimi
pia nikaamua kuwaaga wale ndugu na hivyo nikatafuta pikipiki hapo ikanipeleka mpaka
mitaa ile ambapo nilikuwa na kazi kesho yake. Sikutaka kufikia kwa watu wala
mbali sana na eneo nililoelekezwa kuwa ndio yatafanyika yale yaliyonileta
katika mji huu.
Basi
tulienda mpaka maeneo yale, nikafika mpaka ulipo ukumbi na hapo nikaachana na yule
aliyenipeleka, hivyo ikanibidi nianze kuulizia maeneo hayo kama kuna hoteli ama
mahali pa kufikia, hivyo nikaanza kuzunguka hapo mtaani kuona zilizopo, lakini
mara nilijikuta kwenye mtaa Fulani ambao nilielekezwa hoteli moja hivi ambayo
ilikuwa ni ghorofa na kwa maeneo hayo hiyo ndio ilikuwa na hadhi ya kujielewa,
basi nikawa natembea kuelekea kwenye hoteli hiyo, nilipoikaribia hiyo hoteli
nilishtuka sana maana yalisikika mayowe makubwa sana toka chumbani, na hakuna
aliyekuwa na hakika haswa kunanini ama kuna nani humo ndani!
Nilisimama
kwa muda nione kama watu wengine wanaopita wanasikia ninavyosikia ama ni mimi
peke yangu ndio naona maluweluwe!
Ni ajabu na
kweli kuwa kila aliyekatisha maeneo hayo,aligeuka huku na kule na kuendelea na
safari,na wengine walionesha kama kusonya vile ama kupuuzia kana kwamba
wamezoea kusikia!
Nimezoea
kusaidia watu na hivyo hapa ikanipa tabu sana, nawezaje kwenda wakati kuna mtu
anahitaji msaada? Basi nikabaki njia panda kama nisogee vile au nisimame au
niondoke vile!
Kwakuwa
nilikuwa mgeni maeneo hayo,basi nikaendelea na ile adhma ya moyoni mwangu ya
kutafuta mahali pa kulala,na nilipomuuliza mama mmoja aliniambia kuna
hoteli(lodge) tu maeneo haya,akasema "Ni hiyo hapo,ila zunguka kule mbele
ndio kuna geti" basi nikaanza kujongea mbele na akili ikawa inanituma
kuniambia nikiwa hapo nitajua siri ya makelele hayo!
Nimechoka
sana na safari na natamani kupumzika aisee; Nikaona mlango wa mapokezi,
nikatembea mpaka kwake, Nikamuuliza Kaka napata chumba,akadakia haraka
"Poa kaka,karibu,nafasi zipo...Je unataka full au passport?" Mmh!
Ndio nini sasa? "Namaanisha unataka usiku mzima au unaondoka muda sio
mrefu?" Maswali gani hayo kaka ya kishenzi? Unaona nina begi,huwezi kuhisi
mimi ni mgeni? Na unataka niondoke baada ya muda mfupi,Unaona nafanana na
majambazi au Wanga? "Aah samahani kaka,basi keti hapo subiri wahudumu
wakifanyie usafi fasta,Ni 30,000 tu" Nilikaa pale kando nikiwa nawaza,haya
maeneo ni gani? Kwanza nimesikia mayowe na watu hawaonyeshi kuhali wala
kusaidia na hapa napewa hadithi za kishenzi...ina maana hapa Chumba
kinaandaliwa mgeni akifika tu au? Ama chumba kinaandaliwa kutokana na muda
unaokaa,basi nikaendelea kusubiri!
Basi mara
nikiwa kama nasinzia vile, nikashituliwa na yule mhudumu kaka tayari,naomba
mfuate huyo dada akuonyeshe chumba hapo ghorofa ya pili,basi nikaainuka
nakuanza kupanda,nikiwa napanda ngazi, nikapishana na mtu kama namfahamu
vile,sijui ni nani! Ila nahisi ni mtu mmoja maarufu na yamkini nimewahi kumuona
mahali,sema sina hakika sana yamkini nimefananisha maana alikuwa amevaa
Kofia,wakati namwazia huku naendelea kutembea mara juu kabisa kwenye ile korido
ya kuelekea chumbani kwangu,nikagongana uso kwa uso na binti mmoja aliyekuwa
anajaribu kujifunika ili asifahamike akifika chini, na aliponiona akaishiwa
pozi,nikasikia tu "Aaah Uncleee, Shikamooo,mambooo,Bwana asifiwe!"
Sasa nikiwa bado nawaza huyu ni nani vile,basi nikatabasamu tu, na kusema
Okeeeey Poa!
"Kaka
chumba chenyewe ndio hiki" Alisema yule mhudumu,basi nikajikuta namwambia
yule binti "Haya naona uko na yako, basi sawa..mimi ndio nimefika,nimeona
nipumzike hapa leo, Wewe uko chumba gani
uncleee?"
Aaah Hapana
mimi aaaah bye bwana!
Basi
akashuka haraka akiwa kama amepaniki vile na mimi nikamwangalia akishuka chini
na nikaangia ndani na kuweka mizigo yangu, Lakini mle chumbani nikagundua
hakuna Taulo wala sabuni na nilipojaribu kupiga simu nikaona kama ni mbovu
vile, nasi nikaamua nishuke chini,niombe taulo,sabuni,nichukue chakula na
kulipa pia kuandika taarifa zangu pale mapokezi!
Basi wakati
nashuka nikamkuta tena yule binti pale mapokezi akidai mzigo wake,sasa
ikanibidi nipitilize kwanza kwenda wanakouza chakula,kisha nimalizie
hapo...basi ninaporudi akawa ameshaondoka,Sasa nikiwa pale mapokezi nikamsikia
yule kijana wa mapokezi akisema "Mabinti wengine jamani! Sijui wanakosa
nini aisee?" basi nikadakia "Kwanini kaka?"
Basi
akashusha pumzi na kusema "Kaka wewe acha tu,mambo mengine ni magumu sana
kuamini ila hapa wanakuja Watumishi mbalimbali, wahubiri na hata waimbaji
kadhaa wa injili na watu wengine maarufu,hapa ndio kijiwe chao....Na hata huyu
binti aliyetoka hapa, Nasikia ni Mtoto wa..........ITAENDELEA!!
(c)King
Chavvah, 2015
+255 713
883 797
Instagram;
kingchavvah
Twitter
@kingchavala
Monday, May 25, 2015
LAUGH AGAIN CONCERT.....NYANDA ZA JUU KUSINI IMEANZA VEMA SANA!
Nehemia Hango (Mc Ben)....Upcoming Comedian! |
Princes Hilda Chavala katika pozi la picha |
King Chavala na Dr L Maboko |
Wadau wa Tamasha katika picha!
wacha weeeeeee
Ninaubariki Uchumba huuu kama Uko serious lakini!
Watu wakacheka na kucheka kisha kucheka tena!
Baba Triple J nayeye alikuwepo aiseeee |
I need Space aiseeeee
Queen Happiness wa Chavala kati |
Freppiness Royal Family |
King and Queen Chavala |
Add caption |
Irene nayeye alikuwepo! |
TUNAMSHUKURU SANA MUNGU KWA KUTUWEZESHA KUFANIKISHA SHUGHULI HII, AHSANTE KWA MAPOKEZI MAZURI YA LACS MBEYA NA NYANDA ZA JUU KUSINI!
AHSANTE KWA KILA ALIYESHIRIKI KWA NAMNA YEYOTE ILE!
Hotline 0713 883797
Tuesday, August 26, 2014
MSIONE KIMYA AISEE,NAJIANDAA KUOA MWENZENU 25/10/2014
HABARI ZENU BHANA!!
KWELI NIMEWAMISS MNO MNO, NA MNAWEZA KUWA WENGI MNAJIULIZA MBONA CHAVALA AMEKUWA KIMYA ,NI KWELI YAMKINI,LAKINI MBELE YANGU NINA JAMBO MOJA TU KUBWA ,NALO NI KUOA TAREHE HIYO NIMESEMA ,PANDE ZA MBEYA!!
UKIWA KAMA FAN,RAFIKI AU MTU WA KARIBU SANA, UNAKARIBISHWA SANA KUSHIRIKI TUKIO HILI LA MAISHA KWA NAMNA YEYOTE ILE UNAYOWIWA KUSHIRIKI, IKIWA KWENDA NASI MBEYA BASI NI SAWA ,UKITAKA KUCHANGIA FEDHA,VITU AU MAWAZO NA LABDA ZAWADI,UNARUHUSIWA KUTII UTAYARI WA MOYO WAKO!!
NINAWASHUKURU SANA AMBAO HAWAJAACHA KUTUOMBEA NA KUTUUNGA MKONO IPASAVYO NA IKIWA UNA LOLOTE BASI NI SAWA
0713 883 797(TIGO PESA) AU
0753 883 797(M-PESA)
UNAWEZA NIFUATA FACEBOOK facebook.com/chavalapf
KWELI NIMEWAMISS MNO MNO, NA MNAWEZA KUWA WENGI MNAJIULIZA MBONA CHAVALA AMEKUWA KIMYA ,NI KWELI YAMKINI,LAKINI MBELE YANGU NINA JAMBO MOJA TU KUBWA ,NALO NI KUOA TAREHE HIYO NIMESEMA ,PANDE ZA MBEYA!!
UKIWA KAMA FAN,RAFIKI AU MTU WA KARIBU SANA, UNAKARIBISHWA SANA KUSHIRIKI TUKIO HILI LA MAISHA KWA NAMNA YEYOTE ILE UNAYOWIWA KUSHIRIKI, IKIWA KWENDA NASI MBEYA BASI NI SAWA ,UKITAKA KUCHANGIA FEDHA,VITU AU MAWAZO NA LABDA ZAWADI,UNARUHUSIWA KUTII UTAYARI WA MOYO WAKO!!
NINAWASHUKURU SANA AMBAO HAWAJAACHA KUTUOMBEA NA KUTUUNGA MKONO IPASAVYO NA IKIWA UNA LOLOTE BASI NI SAWA
0713 883 797(TIGO PESA) AU
0753 883 797(M-PESA)
UNAWEZA NIFUATA FACEBOOK facebook.com/chavalapf
Wednesday, July 9, 2014
Monday, June 9, 2014
COMING SOON ON 13TH JULY 2014......LAUGH AGAIN CONCERT....Chavala Hatimaye!!!!
Siku utakayoanza kupambana na Opinions za watu kuhusu wewe na ukasahau kuwa unazo Facts za kutosha kuhusu wewe mwenyewe, hapo ndio utakuwa umeacha kuishi maisha yako halisi na umeanza kuishi maigizo!!
Ukijitambua sawa sawa hutajitahidi kuishi ukiwaonyesha watu jinsi uishivyo ila utajitahidi kumpendeza Mungu na walimwengu sawa sawa na vipimio vya ki-Mungu!! Unapombana na binadamu mwenzio kwa sababu yeyote ile inaonesha kuwa wewe ni MUOGA na unadhani kupambana na wengine ndio kunaweza kukufanya uwe juu, Au huna jambo la maana la kufanya na ndio maana unapata hata muda wa kupambana na wenzio na Au ni Ujinga tu uliochanganyikana na utoto ambao mpaka ukutoke itachukua muda sana!!
Yaani kupigana au kushindana na mwenzio ni sawa na kijiko kiwe na ugomvi na uma au sahani igombane na flampeni kabatini la vyombo hali vyote viko chini ya mwenye nyumba na kila kimoja kimenunuliwa kwa kazi yake na mwenye navyo ndio huamua kipi kifanye nini,kikae wapi na kitupwe lini....sisi sote ni uumbaji wa Mungu,sasa tusemane au kupigana au kushindana ili iweje????/
Nina mengi sana ya kufanya na maisha yangu,yako mengi yananingoja kutimiza na naona muda hata haunitoshi, Ahsante mungu kwa afya njema na akili timamu na msimamo wenye nidhamu katika wewe!
MUHIMU KWA KILA MT:
Tumia muda wako vema na kila siku fanya bidii kutimiza ndoto zako, dini na ujinga havitakufikisha popote, hebu jitafakari tena unatumiaje muda wako!! na ukiona unatumia muda mrefu kufuatilia sijui nani kafanya nini na unatamani kama ungepambana basi ujue una matatizo na ukiendelea hivyo utapotea na kusahaulika kabisa!!!!
Serious people have serious issues to deal with and not other people!!
Think outside the box and be Yourself!!
Ukijitambua sawa sawa hutajitahidi kuishi ukiwaonyesha watu jinsi uishivyo ila utajitahidi kumpendeza Mungu na walimwengu sawa sawa na vipimio vya ki-Mungu!! Unapombana na binadamu mwenzio kwa sababu yeyote ile inaonesha kuwa wewe ni MUOGA na unadhani kupambana na wengine ndio kunaweza kukufanya uwe juu, Au huna jambo la maana la kufanya na ndio maana unapata hata muda wa kupambana na wenzio na Au ni Ujinga tu uliochanganyikana na utoto ambao mpaka ukutoke itachukua muda sana!!
Yaani kupigana au kushindana na mwenzio ni sawa na kijiko kiwe na ugomvi na uma au sahani igombane na flampeni kabatini la vyombo hali vyote viko chini ya mwenye nyumba na kila kimoja kimenunuliwa kwa kazi yake na mwenye navyo ndio huamua kipi kifanye nini,kikae wapi na kitupwe lini....sisi sote ni uumbaji wa Mungu,sasa tusemane au kupigana au kushindana ili iweje????/
Nina mengi sana ya kufanya na maisha yangu,yako mengi yananingoja kutimiza na naona muda hata haunitoshi, Ahsante mungu kwa afya njema na akili timamu na msimamo wenye nidhamu katika wewe!
MUHIMU KWA KILA MT:
Tumia muda wako vema na kila siku fanya bidii kutimiza ndoto zako, dini na ujinga havitakufikisha popote, hebu jitafakari tena unatumiaje muda wako!! na ukiona unatumia muda mrefu kufuatilia sijui nani kafanya nini na unatamani kama ungepambana basi ujue una matatizo na ukiendelea hivyo utapotea na kusahaulika kabisa!!!!
Serious people have serious issues to deal with and not other people!!
Think outside the box and be Yourself!!
Tuesday, April 22, 2014
HII NI SERIOUS KABISA, MWAKA HUU KING CHAVALA ANAOA!!
JUMATATU YA JANA NDANI YA HEMA KING CHAVALA AMEWEKA WAZI JINSI ILIVYOKUWA KWAKE CHANGAMOTO KUOA LAKINI HATIMAYE MWAKA HUU ANAOA, AMESEMA TAREHE 20 YA JULY NDIO ATAKUWA ANAMDHIHIRISHA MREMBO HUYO MBELA YA UMMA NA SIKU HIYO HIYO PIA ATAKUWA NA TAMASHA KUBWA KATIKA MFULULIZO WAKE WA MATAMASHA YA COMEDY....LAUGH AGAIN CONCERT....Chavala Hatimaye!!
BASI TUNGOJEE ILI TUJUE YUKO SERIOUS KWELI AU NI COMEDY AS USUAL!!!
BASI TUNGOJEE ILI TUJUE YUKO SERIOUS KWELI AU NI COMEDY AS USUAL!!!
Subscribe to:
Posts (Atom)