![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhqfYZlYx40usqGCi7bmj8nzQ9bxHfcd8keOOrSQD_vnScd0C0GqF25ULyMnZmbZYrKkHY8MrFR4fiqCctY_EuAIkyg25ND_Y-WD3pPpfx333B7ic7uDsKoWeEbUPjaUxzXw6zuDLs7ESY/s1600/clown.jpg)
Habari zenu tena, ndugu wasomaji!!
Kwa mara
nyingine tena natamani ucheke kidogo na kuongeza siku zako za
kuishi,Najua unaangaliaga filamu/movie tena zile za kutisha sana kama
vile za mazombie na mavampire...lakini hivi karibuni nimegundua hakuna
Movie kali zaidi ya Biblia,kwanza star ni Mungu mwenyewe na mastar
wasidizi unaweza hata kuwa wewe ukitaka,lakini kama unakumbuka Jinsi
ambavyo Samson aliua watu zaidi ya laki nne nae akafa nao...wewe umewahi
kuona movie kama hiyo? Vipi shadrack ,meshack na Abeidnego walivyopita
kwenye moto bila kuungua na hapo hamna cha kompyuta wala nini,maana hizi
movie zingine huwa watu wanatengeneza tu kwa kompyuta....na mwisho wa
Biblia kuna script ambayo bado haijachezwa aisee inatisha,yaani
mavampire na mazombie hayaingii hapo hata kidogo hi wewe umewahi kuona
ng'e kama farasi,si ninakuuliza wewe?
No comments:
Post a Comment