Baada ya kufanya Tamasha la KUCHEKA TENA la
mwisho pale Landmark Hotel,Ubungo mwezi wa tatu na hatimaye Arusha mwanzoni mwa
June hatimaye mkali na muasisi wa christian comedy nchini Tanzania anatua tena
jijini Dar es salaam kwa Tamasha lake la nne toka ameanza mwishoni mwa mwaka
jana pale Ubungo plaza.
Yaani ni kucheka na kucheka na kucheka tena
huku ukimsifu Mungu na kujifunza yapasayo kutenda katika maisha yako ya utauwa.
Tamasha hili litawasimamisha Up Coming
Comedians wa kutosha katika segment maalum ya OPEN MIC, na wale ambao
wamezoeleka kama Richard Chidundo,Gerald Mrema,pilipili,Josephine na wengine watakuwa
sambamba na waimbaji kama Sarah Shila, Deogratius, Meshack, Gee & Seth, WordAlive
and Dar es salaam Gospel Bands,Golden Eagles and 1st Q dance groups
katika kunogesha na kuhudumu pamoja na Mkali wa jukwaa, mtu aliye dawa.....The
King Of Stand Up Comedy,CHAVALA.
Kwa wale wafuatiliaji wa mambo, naamini
LAUGH AGAIN CONCERT SERIES sio jambo geni masikioni mwao!!
Huu ni ule mfululizo maalum wa matamasha ya
vichekesho na vipaji halisi vya kikristo hapa nchini ambao unasimamiwa na
MC/Comedian na Muasisi wake nchini CLOWN CHAVALA(The King of Stand Up Comedy)
kupitia Chavala Ideas Platform chini ya udhamini mkubwa wa Great Potentials
Ltd.
TAMASHA HILO LITAANZA SAA TISA JIONI MPAKA
SAA MOJA NA NUSU USIKU(3-7:30PM)
NA KIINGILIO KITAKUWA 5000/=
NA 2000/= TU KWA
WATOTO.
Katika SERIES hii bado tuko Msimu(SEASON)
wa kwanza na hili Tamasha lijalo litakuwa Tamasha la tatu kwa Dar es
salaam na ni Episode II. Kama
ilivyotaarifiwa mapema Tamasha hili la jpili ijayo(24th June 2012)
pamoja na mawili yafuatayo kwa hapa Dar(Yaani Tar 23th Sept na 23/30th
Novemba-mkesha wa mwisho) yatafanyika katika
ukumbi wa CITY CHRISTIAN
CENTRE-UPANGA(Mkabala na Mzumbe Dsm)
TAMASHA HILI LIMEDHAMINIWA NA GREAT
POTENTIALS LTD,CITY CHRISTIAN CENTRE(CCC),TOUCHING
VISION,AUTHOR2READERS,WORDALIVE CHURCH,OLYMPUS COMPUTERS AND CHAVALA IDEAS
PLATFORM.
Akielezea mafanikio yaliyopatikana Chavala
amesema;.....Kwa kweli mafanikio ni makubwa sana mpaka sasa ingawa mengine
hayawezi kuonekana kwa macho ya nyama ila itoshe tu kusema mafanikio ni makubwa
mno;yaani toka kule ambako nilikuwa sitambuliki na watu kwa makusudi walikuwa
hawataki kuona umuhimu wa Comedy katika ulimwengu wa kikristo mpaka sasa ambako
wengi wameanza kuelewa, wamepokea na wamekubali,kibali nilichokipata Arusha kwa
mfano ni kikubwa mno kiasi cha kushangaza; kwa sasa nina vijana wengi sana
ambao wamevutwa na kuona nao wanaweza kumtumikia Mungu kwa vipaji vyao kama
vile Comedy,Dance na Mashairi na mengine mengi ya vipaji halisi, hivyo nina
wanafunzi wakutosha na zaidi washika dau,wachangiaji na wanaounga mkono ni
wengi sana na hata wewe unaesoma hapa unakaribishwa kuwa mmoja wao.
Nimeongeza marafiki na maadui(ingawa kwangu
ni invalid) na nimekuza network base yangu hapa nchini, kwa msaada wa media
ninaamini nitaweza kuyafikia majiji yote nchini na kutambulisha Christian
Comedy na vipaji halisi isipokuwa Tanga peke yake,ambayo haiko katika ratiba ya
msimu huu w kwanza.
Chavala ametoa ratiba yote ya mwaka
iliyobaki kuwa anatarajia kufanya Matamasha makubwa hayo katika majiji yote ya
Tanzania kabla ya Novemba,mpaka sasa matamasha hayo yameshafanyika Dar es
salaam na Arusha na Mwishoni mwa July Chavala atakuwa Mbeya,mwishoni mwa August
itakuwa Mwanza,September ni Dar tena,October itakuwa Dodoma na Mwisho wa
Novemba nitamalizia kwa mkesha pale CCC-Upanga,huu utakuwa ni mkesha maalum wa
kumaliza msimu wa kwanza na utahusisha wasanii wote na wengine wateule ambao
wamepata nafasi ya kushiriki katika matamasha mbalimbali ya msimu huu wa
kwanza!!
Kwa matamasha yote hayo yaliyo mbele bado
kuna mengi na vingi vinahitajika,kama vile Pesa, Laptops,Kamera,Music
system,Sudio na mengine mengi hivyo ikiwa unaguswa
kuhusika/kuchangia/kudhamini/kushauri chochote katika Tamasha lolote wakati
wowote tafadhali usisite kufanya hivyo, tutashukuru mno ingawa tunashikilia
haki ya kutendea kazi au kutunza ushauri wowote ule ujao toka nje.
Unaweza kutuandikia kupitia lacs.project@gmail.com
au tupigie kupitia +255-(713/753)-883
797....pia unaweza kuchangia kwa benki za simu(M-pesa na Tigo Pesa) kupitia
no.hizo hizo.
Lakini pia unaweza kutembelea blogs
1.
www.gospelstandardbase.blogspot.com......hii
ina mafundisho zaidi kuhusu Neno la Mungu toka kwa watumishi wa Mungu
mbalimbali
2.
www.chavalapf.blogspot.com.......hii
inahusika na mawazo mbalimbali ya watu mbali ambayo ni muhimu na yanajenga!
3.
www.kingchavala.blogspot.com......
Hii ni maalum kwa ajili ya shughuli zote na matukio yote yamuhusuyo Clown
Chavala,The King!
Na unaweza kutembelea page ya facebook;
LAUGH AGAIN CONCERT SERIES
Au page mahususi ya Chavala...
www.facebook.com/KingChavala au www.facebook.com/chavalapf na
zaidi wale watumiaji wa Twitter mnaweza kumfuataPresident Chavala @ClownChavala
ANGALIZO;
Kama ungetamani kuwa mwanachama na unapenda
kupata habari kila mara zikiwepo huhusu mizunguko ya Chavala katika kampeni hii
na kufanyika kwa matukio haya kokote kule nchi usisite kutuandikia kwa e-mail
hiyo hapo juu.
Na kwa wale wasanii wanaochipukia na wale
wanaofahamika huko mikoani tafadhali wasiliana nasi mapema kama ungependa
kushiriki katika mojawapo ya matamasha haya kwa namna yeyote ile.
SHUKRANI;(Na President Chavala)
Mwisho napenda kutoa shukrani kwa mashabiki
na wafuasi wangu wote ambao ndio wanafanya jambo hili liiendelee kukuwa siku
hadi siku,tunashukuru kwa wachangiaji wa fedha,mawazo,muda na ujuzi;
ninawashukuru wote wanaotuombea na kututakia mema kila wakati majukumu
haya;Ahsante kwa magazeti,ahsante watumiaji wa Social networks kama
Twitter,facebook na blogs na wanahabari wote zaidi redio,magazeti na christian
blogs,kuanzia wanahabari binafsi mpaka wale wanaofanya kwenye makampuni na
Taasiss binafsi na za serikali ambao mmkekuwa mstari wa mbele katika kupigia
debe jambo hili! Naamini Mungu lazima awalipe katika mambo yenu!
Natambua mchango wa wasanii wengine katika
sanaa hii, maana peke yangu nisingefika popote pale,ahsanteni Emmanuel
Mgaya(Masanja Mkandamizaji); Evance Bukuku(VuvuZela Comedy Show); pamoja na
vijana wangu kama Richard Chidundo;Mrema Gerald, Senior ABBy na MC
Manu/pilipili toka Dodoma na wengine wengi ambao kimsingi mchango wao
unatambulika!
Naamini kila utakapoona tangazo popote
hautasita kufika na kuwaalika wengine au wenzako...tafadhali anza kutekeleza
hayo na Tamasha hili,ubarikiwe sana!!
Unaweza tembelea facebook group yetu ;
http://www.facebook.com/groups/lacs.project
Unaweza tembelea facebook group yetu ;
http://www.facebook.com/groups/lacs.project
Ahsanteni sana na karibuni sana sana
kucheka tena na tena na tena maana kucheka ni dawa na kunaondoa sumu mwilini!!