Tuesday, June 25, 2013

HAKUNA MOVIE KALI KAMA BIBLIA AISEEE!!!

Habari zenu tena, ndugu wasomaji!!
Kwa mara nyingine tena natamani ucheke kidogo na kuongeza siku zako za kuishi,Najua unaangaliaga filamu/movie tena zile za kutisha sana kama vile za mazombie na mavampire...lakini hivi karibuni nimegundua hakuna Movie kali zaidi ya Biblia,kwanza star ni Mungu mwenyewe na mastar wasidizi unaweza hata kuwa wewe ukitaka,lakini kama unakumbuka Jinsi ambavyo Samson aliua watu zaidi ya laki nne nae akafa nao...wewe umewahi kuona movie kama hiyo? Vipi shadrack ,meshack na Abeidnego walivyopita kwenye moto bila kuungua na hapo hamna cha kompyuta wala nini,maana hizi movie zingine huwa watu wanatengeneza tu kwa kompyuta....na mwisho wa Biblia kuna script ambayo bado haijachezwa aisee inatisha,yaani mavampire na mazombie hayaingii hapo hata kidogo hi wewe umewahi kuona ng'e kama farasi,si ninakuuliza wewe?
Kuna mabadiliko mengi sana tangu zamani,leo na wakati ujao....zamani tulikuwa tunaangalia movie na wazazi na ikifika mahali pabaya basi Baba alikuwa anapeleka mbele haraka....ila siku hizi mambo yamegeuka....Watoto ndio wanamwambia Baba yao..."Baba hapo peleka mbele...mhh" sasa unajiuliza hapo nani anapaswa kumchunga mwenzake..mtoto au mzazi!!
Nimalizie sehemu hii kwa kuwauliza swali.....Nimesikia Edson akiimba...Ni kwa neema tu....na wimbo huo umekuwa maarufu sana,ila mle ndani anasema....Nimetoka mbali..X3,sasa nilipoulizia watu kuwa huyu ndugu anatokea wapi...Wakaniambia anasali Kijitonyama....SASA NASHANGAA,JAMANI KWELI KIJITONYAMA NI MBALI??
http://kingchavala.blogspot.com

No comments:

Post a Comment