Saturday, June 29, 2013

NILIBAHATIKA KUHUDHURIA "LADIES OF DESTINY OVERCOMERS NIGHT"!!!

KING CHAVALA ON THE  STAGE
HABARI YAKO!!!
IJUMAA YA JANA NILIBAHATIKA KUHUDHURIA USIKU MAALUM ULIOPEWA JINA...."LADIES OF DESTINY OVERCOMERS NIGHT" TUKIO HILI LA MKESHA LILIWALENGA SANA WANADADA INGAWA LILIKUWA WAZI KWA WOTE....KWA WAO KUJIFUNZA KUHUSU WAO NA SISI WANAUME KUJUA NAMNA YA KUBEBANA NA YALE YATUPASAYO!!!
UMATI WA WAHUDHURIAJI WAKIWA WAMEZAMA KUABUDU
KWA HAKIKA MKESHA ULIKUWA MZURI SANA NA ULIFANYIKA KATIKA THEATRE YA MAKUMBUSHO PALE POSTA MKABALA NA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA(IFM)....MKESHA HUO ULIANZA SAA NNE USIKU MPAKA KUMI NA MOJA ASUBUHI!!
ROSE MUSHI....MBEBA MAONO

WATU WALIOPATA NAFASI YA KUSEMA NI PAMOJA NA ROSE MUSHI(MBEBA MAONO),FARAJA KOTA(MWANASHERIA NA ALIYEWAHI KUWA MISS TANZANIA); PHILIP FRANK PAMOJA BROTHER KINGU(KIJANA ALIYEOA HIVI KARIBUNI)!!
MISE ANAEL....MZEE WA XAXAPHONE

FARAJA KOTA....MMOJA YA WAZUNGUMZAJI

BROTHER KINGU....MNENAJI ALIYEHITIMISHA

ISACK MALONGA

FRANK PHILIP....MMOJA YA WANENAJI

PAPAA SEBENE NAE HAKUKOSA TUKIO HILO

MKESHA HUO ULIHUDUMIWA NA GLORIOUS CELEBRATION TEAM, MISE ANAELI(MZEE WA XAXAPHONE); 1ST Q DANCER PAMOJA NA MIMI KWA UPANDE WA STAND UP COMEDY!!
NI MWENDO WA KUSEREBUKA TU

1ST Q DANCERS NAO WALIKUWEPO JUKWAANI USIKU HUO

HAKIKA KUNA UPEKEE KATIKA CHOMBO HIKI

MCHUNGAJI TIM OTHY KYARA PAMOJA NA MKEWE,PAPAA SAMUEL SASALI, ISACK MALLONGA NI BAADHI YA WATU MUHIMU KABISA WALIOTOKEA KATIKA USIKU HUO WA KWANZA KUANDALIWA NA LADIES OF DESTINY NETWORK!!!
...MUNGU YUKO HAPA

...HAKIKA YEYE NI MUNGU TU

ROSE NA CHAVALA JUKWAANI

 ....HAYA TUCHEZE STAILI IPI?
JAMANI ROSE MBONA HUNIJIBU?
HAPO SAWA!

MKESHA HUU ULIENDESHWA NA MC CAROLYN!

BINAFI NINAMPONGEZA SANA ROSE MUSHI KWA HATUA NZURI ALIYOANZA NAYO NA NINAAMINI TUKIO HILI LITAKUWA LA KIMATAIFA,LITAKUWA LIKIFANYIKA ZAIDI YA SIKU MOJA NA SIO USIKU NA LITAENDA LIKIBOREKA NA KUWA LA MAANA KWA JAMII YOTE!!!
 ....HAPA JE UNAONAJE? TUMEPENDEZA AU TUBADILI POZI LA PICHA?
ROSE MUSHI,FARAJA KOTA NA KING CHAVALA

PRESS ON!!!

  
MA-MC WENYE MATABASAMU YA VIWANGO!!!
KUMBE SISI NI PHOTOGENIC EEEHHH!!!?

AHSANTE SANA!
 BY KING CHAVALA
+255 713 883 797

Tuesday, June 25, 2013

HAKUNA MOVIE KALI KAMA BIBLIA AISEEE!!!

Habari zenu tena, ndugu wasomaji!!
Kwa mara nyingine tena natamani ucheke kidogo na kuongeza siku zako za kuishi,Najua unaangaliaga filamu/movie tena zile za kutisha sana kama vile za mazombie na mavampire...lakini hivi karibuni nimegundua hakuna Movie kali zaidi ya Biblia,kwanza star ni Mungu mwenyewe na mastar wasidizi unaweza hata kuwa wewe ukitaka,lakini kama unakumbuka Jinsi ambavyo Samson aliua watu zaidi ya laki nne nae akafa nao...wewe umewahi kuona movie kama hiyo? Vipi shadrack ,meshack na Abeidnego walivyopita kwenye moto bila kuungua na hapo hamna cha kompyuta wala nini,maana hizi movie zingine huwa watu wanatengeneza tu kwa kompyuta....na mwisho wa Biblia kuna script ambayo bado haijachezwa aisee inatisha,yaani mavampire na mazombie hayaingii hapo hata kidogo hi wewe umewahi kuona ng'e kama farasi,si ninakuuliza wewe?
Kuna mabadiliko mengi sana tangu zamani,leo na wakati ujao....zamani tulikuwa tunaangalia movie na wazazi na ikifika mahali pabaya basi Baba alikuwa anapeleka mbele haraka....ila siku hizi mambo yamegeuka....Watoto ndio wanamwambia Baba yao..."Baba hapo peleka mbele...mhh" sasa unajiuliza hapo nani anapaswa kumchunga mwenzake..mtoto au mzazi!!
Nimalizie sehemu hii kwa kuwauliza swali.....Nimesikia Edson akiimba...Ni kwa neema tu....na wimbo huo umekuwa maarufu sana,ila mle ndani anasema....Nimetoka mbali..X3,sasa nilipoulizia watu kuwa huyu ndugu anatokea wapi...Wakaniambia anasali Kijitonyama....SASA NASHANGAA,JAMANI KWELI KIJITONYAMA NI MBALI??
http://kingchavala.blogspot.com

MJUE....MC/COMEDIAN GERALD MREMA....a.k.a NYUKI WA BWANA!!!

MC/Comedian GERALD MREMA
 BADO TASNIA YA UCHESHI NCHI NI CHANGA NA INAENDELEA KUKUA NA KWA UPANDE WA KANISA SANAA HII INAENDELEA KUFANYA VEMA SANA, KIPEKEE NATAMANI NIMTAMBULISHE MC/COMEDIAN MWINGINE KUTOKA LAUGH AGAIN CONCERT SERIES ENTERTAINMENT, HUYU NI MMOJA YA VIJANA AMBAO NILIANZA NAO TANGU SIKU YA KWANZA YA MFULULIZO HUU

 MNG'AO WAKE NI MKUBWA SANA INGAWA BADO WENGI HAWAJAMUELEWA,BILA SHAKA WANAFUNZI WENGI WA VYUO VIKUU KATIKA SHUGHULI ZAO NYINGI WAMEKUWA NAE NA BADO WANAENDELEA KUMTUMIA VEMA MAANA ANAELEWEKA VIZURI SANA NA KUNDI HILO.....HUYU NI MSOMI ALIYEHITIMU SHAHADA YAKE YA KWANZA KATIKA CHUO KIKUU ARDHI NA SASA NAFANYA KAZI NA KAMPUNI BINAFSI KAMA MTHAMINI MAZINGIRA
KWENYE MAHAFALI NA MATAMASHA MBALI HUKO VYUONI AMEKUWA MC ANAYEHITAJIKA SANA,NA HUYU NDIYE ALIYELETA MISEMO KAMA VILE....ipo shida....Mungu akutie nguvu.......Maua na nyuki wa Bwana na mengineyo mengi...KWA HAKIKA KIJANA HUYU ATIWE NGUVU!!
BILA SHAKA MTAMUONA HIVI KARIBUNI KATIKA KAZI ZETU NYINGI ZINAZOKUJA!!
PAMOJA SANA!!!
Connect nae kwa facebook;
http://www.facebook.com/Scientist.Gerald.Don.Mrema
NA KAMA UNAMWITAJI KWA SHUGHULI BASI 0714254900

LAUGH AGAIN SERIES.....We make you Laugh, Relax and Release yourself!!!
By KING CHAVALA-MC
Hotline 0713 883 797

HATIMAYE PAPAA ATHIBITISHA NA KUANIKA ALIYEMWANGUSHA!!!

HABARI ZENU BASI!
BAADA YA SARAKASI NA MISERELEKO YA MUDA MREFU YA KIJANA FULANI MTANASHATI, MREFU SANA HUSUSANI UKIMLINGANISHA NA YEYE MWENYEWE,MSHEREHESHAJI,MTANGAZAJI NA MTU WA MAMBO MENGI MJINI,JUMAPILI HII AMETHIBITISHA NA KUWEKA WAZI BINTI ALIYEBAHATIKA KUMWANGUSHA KWA PIGO MOJA TU....MMMH HUYU HAPA NI MILEMBE MADAHA!!
FUATANA NAMI KATIKA PICHA UONE SIKU HIYO ILIKUWAJE.....
KUBEBWA KULIANZIA NDANI KISHA AKATOLEWA NJE JUU
HATIMAYE NDANI WATU WALIMBEBA KAMA NINI....
....VAA PETE HII KAMA ISHARA NA ALAMA YA UCHUMBA WETU.....
.....HATA KAMA ANGEKUWA NANI LAZIMA ANGECHEKA TU!!
....NA MILEMBE NAE AKATOA NADHIRI...
MCHUNGAJI DK HURUMA NKONE AKIWAOMBEA 
HATIMAYE MCHUNGAJI AKAWATANGAZA KAMA WACHUMBA RASMI SASA
.....PAPAA AKIONGEA KABLA HAJATOA SHUKRANI YA PEKEE
HAWA NI WANA FAMILIA YA SASALI WALIOKUWEPO PAMOJA NA MZEE SASALI
CHAKULA MAALUM CHA MCHANA,KAWE BEACH
MEZA YA MARAFIKI WAKILA PAMOJA
SAMUEL AKIMTAMBULISHA MCHUMBA WAKE NYUMBANI
WACHUMBA WAKIPIGA STORI MBILI TATU WAKATI WA CHAKULA
BASI SHUGHULI HIYO ILIKUWA BOMBA SANA MAANA MARAFIKI WENGI WALIJITOKEZA KUMUUNGA MKONO...PICHANI UNAWAONA NAFTALI,PAPAA,SILAS MBISE,JIMMY TEMU,MATHEW NA WENGINEO AMBAO HAPA PICHANI HAWAJATOKEA!!!

HONGERA SANA PAPAA THE BLOGGER KWA HATUA HII!!!

BY KING CHAVALA-MC
0713 883 797

Thursday, June 20, 2013

"MOVIE DHAHANIA YA BIBLIA NA VISIBLE VOICES"

MC CHAVALA +255 713 883 797
 YAMKINI KICHWA CHA HABARI KIMEKUTISHA,LAKINI NIMEEMAANISHA KUSEMA HIVYO...VISIBLE VOICES(SAUTI ZINAZOONEKANA)
HII NI HABARI INAYOKUJIA HIVI KARIBUNI PALE ULIPO....YAMKINI UMEWAHI KUANGALIA MOVIE NYINGI SANA LAKINI BADO HUJAWAHI KUZINGATIA BIBLIA KAMA MOVIE,LAKINI HIVI KARIBUNI NITAANZA KUKUELEZEA KIDOGO KIDOGO TUKIONANA HUKO HUKO MATUKIONI!!!
TUKIWA LOCATION NA WADAU WA GOSPEL HITS
 SAUTI NI SAUTI NA INAPASWA KUSIKIKA LAKINI KUNA SAUTI ZISIZO ZA KAWAIDA AMBAZO HAZISIKIKI TU BALI HUONEKANA NA HIZI ANAZO KILA MTU HATA KAMA HAJUI KAMA ANAZO...
KING CHAVALA NA MARAFIKI!!
FUNGUA MACHO YAKO UONE...TENA UONE SAWASAWA NA VILE MUNGU AONAVYO, KWA HAKIKA MUNGU AMETUSAIDIA MNO KUTUPA UFAHAMU WA KUJUA,KUONA NA KUSIKIA MENGI,ILA NATAMANI UPATE HII MOVIE NA UJIFUNZE ZAIDI!!

COOOOOOOOOMING SOOOOOOOOON!!!!

KIJANA MWENYE KIPAJI,TUMIA FURSA KAMA HIZI KUKUZA KIPAJI CHAKO!!!

KWA SIKU ZA KARIBUNI KUMEKUWA NA MATAMASHA YA KUTOSHA AMBAYO YANATOA FURSA KWA VIJANA WENYE VIPAJI KUONYESHA NA KUKUZA UWEZO WAO,NAAM NASI HUWA HATUKO NYUMA KATIKA KUWATIA MOYO VIJANA HAWA,NAMIMI NATAMANI NIKUTIE MOYO KIJANA,USIKAE CHINI KULALAMIKA TU, TUMIA NAFASI KAMA HIZI ILI UKUE...NG'ANG'ANA TENA SANA,MAANA SIO RAHISI KUKUA KAMA UNATAKA KUPASULIWA YAI!!!!
KILA LAKHERI WAANDAAJI WA "YOUTH TALENTS EXPLOSION CONCERT"

By King Chavala
+255 713 883 797

Monday, June 17, 2013

KING CHAVALA NA WATOTO WA MUNGU JUMAPILI HII YA TAR 23/06/2013!!!!

KWA MOYO MOYO NIMEJITOA KUHAKIKISHA TUKIO HILI JEMA LA UZINDUZI WA DVD YA WATOTO WA MUNGU LINAFANIKIWA NA CHANGIZO KWA AJILI YA WATOTO HAO KUJITEGEMEA NA KUJIENDESHA LINAFANIKIWA!!!!
NJOONI WOTE TUKUTANIKE JPILI HII HAPO UKUMBI WA KANISA LA MAISHA YA USHINDI- UBUNGO EXTERNAL!!
HII INATUHUSU SOTE!!!!

Hotline +255 713 883 797
King Chavala-MC