Monday, October 15, 2012

CHEKA TENA NA KING CHAVALA

 
 .....NASHINDWA KUEREWA...KAMA NI "ERO' YA A'ARA" AMA "ARA" YA "ERO"
NAKUMBUKA NILIPOKUWA SEKONDARI, KULIKUWA NA MWALIMU WANGU WA KISWAHILI AMBAYE NI MWENYEJI WA MKOA FULANI na hizi ndizo zilikuwa zake
(hapa nimeandika kama ambavyo anasikika na cha ajabu yeye ndio mkosoaji)

TATIZO RA RAFUZI YA RUGHA MAMA IMEKUWA SHIDA, WATU WANASHINDWA KUONGEA KISWAIRI KABISA.....YAANI WATU WENGI NAWASHANGAA SANA, ETI KWENYE "ERO" WANAWEKA "ARA" NA KWENYE "ARA" WANAWEKA "ERO"...SASA UNASHINDWA KUEREWA, KUWA WANAMAANISHA "ERO" YA 'ARA" AMA "ARA" YA "ERO".........na kwasababu hiyo hata maneo wanayoyasema YANARETA MAANA ZA MKANGANYIKO; UTAMSIKIA MTU ANASEMA
1."SIRI" SASA UNASHINDWA KUEREWA AMEMAANISHA "SIRI" YA KUGOMA KURA CHAKURA AMA "SIRI" YA KUFICHA MAMBO MOYONI...AU
2."KURA" sasa UNASHINDWA KUEREWA AMEMAANISHA KURA YA KURA CHAKURA AMA KRA YA KUCHAGUA....WHY? KWASABABU ERO NA ARA MNAZICHANGANYA ETI HUYU NAE NAE ANASEMA
3."KARAMU" SASA TUNASHINDWA KUEREWA ANAMAANISHA KARAMU YA SHUGHURI AU KARAMU YA KUANDIKIA!!!
JIFUNZENI KISWAIRI NDUGU ZANGU, HIYO NDIO RUGHA YENU!!!

basi nilikua nachekaje hahahaha na nilivyokuwa ninammiss class!!!!

........NAJUA WENGI MTA-RIKE, LAKINI NASHINDWA KUEREWA MNA-RILE KWA ARA YA ERO AU ERO YA ARA HAHAHAHAH!!

No comments:

Post a Comment