Wednesday, July 24, 2013

KING CHAVALA......NINAWASHUKURU SANA KWA SUPPORT YENU NYOTE!!!

KING CHAVALA COMPLEX
SIO KWA AKILI WALA KWA UJUZI WALA UMAARUFU WALA ELIMU WALA VYOMBO VYA HABARI NA WALA SIO KWASABABU YA FEDHA,ILA MPAKA HAPA NIMEFIKA NI KWA NEEMA TU YA MUNGU!!

NINAMSHUKURU SANA MUNGU KWA KUWA RAFIKI MZURI KWANGU, SIJAFIKA BADO NINAKOKWENDA LAKINI SIKO PIA NILIKUWA, NINAPOKARIBIA KUTIMIZA MIAKA MIWILI YA "LAUGH AGAIN CONCERT SERIES-LACS" MNAMO NOVEMBA 20, NATAMANI NIANZE KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KABISA KWA KILA MTU ALIYE KARIBU NA MIMI NA ALINISAIDIA KWA HALI NA MALI MPAKA LEO NIMEFIKA HAPA.

AHSANTE KWA MICHANGO YA FEDHA NA MAOMBI NA BADO NAYAHITAJI SANA SANA HATA SASA....NINAWASHUKURU SANA WATU WA NGUVU AMBAO TUMEKUWA PAMOJA TANGU MWANZO HATA SASA!!!
INGAWA HATUJAFANYA TAMASHA LOLOTE MWAKA HUU,BASI TARAJIA MAMBO MAKUBWA DECEMBER 1

MUNGU AKUBARIKINI NYOTE MNAOJITOA KWA ROHO SAFI!!!

KING CHAVALA
+255 713 883 797
Facebook; King Chavala

YOUTH KINGDOM MINISTRIES NA SEMINA NYINGINE YA UONGOZI!!


HII NI NAFASI NYINGINE KWA KIJANA WA TANZANIA!
HII NI FURSA YA KIPEKEE YA KUIKIMBIA, MAANA HAUKUNA SABABU YA KUKOSA, JIFUNZE NA JIANDAE KIONGOZI WA KIFALME KATIKA ULIMWENGU WA ROHO!!
NI AUGUST 4, 2013 PALE DEAR MAMA HOTEL,DODOMA KUANZIA SAA SABA MCHANA MPAKA KUMI NA MBILI JIONI!
JIANDIKISHE SASA!! 0712 661842

AHSANTE MUNGU MAANA NAMIMI NITAKUWA MMOJA WA WAZUNGUMZAJI SIKU HIYO!!!

Thursday, July 18, 2013

BREEKING NEWS; AJALI MBAYA SANA YATOKEA HAPA DARAJANI RUAHA!!!

Mungu Wangu, Mungu wangu!!
Yaani madamu yametapakaa kila mahali dah!
Hii ni ajali mbaya sana kuwahi kutokea mwaka katika daraja hili aiseee!
Nakwambia ukiona picha huwezi kutamani kabisa kula nyamna!
Tisa wamekufa hapo hapo,tena wanne wamekatika vichwa na watatu wamevunjika miguu yote miwili na hawa wawili ndio Utumbo uko nje kabisa!
Hawa waliobaki hai ni zaidi ya Ishirini na tano lakini hali zao ni mbaya sana na yamkini tukawapoteza wengine ndani ya hizi siku mbili,hapa kila mmoja amechanganyikiwa na wengine wanajizungusha tu hapahapa huku wakilia na hamna wanachosaidia!
Namshangaa sana Mungu maana katika ajali hii kuna huyu mmoja tu, ambaye ni mdogo yeye ndio hajagugwa wala kuchubuliwa hata kidogo.
Naona Watu wengi wanakazana kusaidia kwa juhudi zote,
lakini wengi wanaogopa sana maana hali inatisha na kuna hatari ya wewe unaesaidia kupata majanga pia!
Ahsante Mungu kuna watu wamejiaminisha na hawaogopi hili awala lile na hawa wamesema hata wakiumia au kufa potelea mbali,bora wamejitoa kusaidia pale wanapoweza!
Na kwa mujibu wa Mashuhuda walioshuhudia ajali hii wanasema imesababishwa na mwendokasi wa dereva na ndio maana ikaleta madhara makubwa namna hii!
Yaani ni bonge la hasara,na kama ndio mtu alikuwa anaanza tu kujikwamua,atakuwa ameumia sana nafsini mwake,Jamani msiache kumuombea maana huwezi jua yanayomsibu!
Lakini pia nafikiri kama ile mikanda ingekazwa wala hayo yasingelitokea na inasemekana walijazwa humo kupita kiasi yaani....lakini watu tunakuwa na uchu wa fedha hivyo mpaka tunalazimisha hata idadi ikipitiliza sisi wala hatujali...ona sasa jinsi ajali hii ilivyoleta foleni,yaani magari ya huku hayaendi wala ya kule hayatembei na haijulikani tutavuka saa ngapi hapa!
Kweli imenisikitisha sana sana maana nasikia vilio tu vya majonzi vya hao waliobaki na unashindwa ufanye zaidi na wewe unashangaa machozi yanakutoka tu......Kwa habari zisizo rasmi nimesikia kuwa huyu dereva wa Lori alikuwa speed sana na aliporuka lile tuta basi tairi la mbele kulia likapasuka na hivyo likamvuta mpaka akaja akagonga ukingo wa kulia wa daraja na ndio hapo sasa lile Tenga waliokuwemo hao kuku likaruka mpaka mbele ya barabara na hivyo msleleko wa Trela ukaja ukapita katikati ya lile tenga kwa upana na ndio hapo wale kuku tisa wakafa vibaya palepale kama nilivyowalezea hapo juu....sasa jinsi lile trela lilivyokaka linaweza kuanguka wakati wowote ule maana linaning'inia juu ya daraja hivyo wananchi wanaogopa kama wakiingia kuwatoa wale kuku wazima linaweza kuwakuta la kuwakuta,na kijana mwenyewe inasemekana mtaji amekopa yaani hapa analia ile mbaya,lakini basi ndio ishatokea...pole yake kwa kweli...........
Babu: Wewe hebu zima hiyo Tv huoni kama mimi napumzika hapa,au wewe unapenda kusumbua tu watu.
(Babu alipoona huyu mjukuu hasikii akaamka na kumfuata,akamnasa bonge la kibao)
(YAANI BABU TU KUMNASA KIBAO YULE MJUU WAKE)
Akashtuka kumbe alikuwa anaota anaangalia Breeking news ya kwenye TV....Dah ndoto zingine bhana!!
****************************************************
(SAMAHANI JAMANI HIVI SCRIPT YA MOVIE IMEKAA VIZURI? TAFADHALI NAOMBA MAONI YAKO KWA AJILI YA MABORESHO)
— in Ruaha, Iringa.

Wednesday, July 3, 2013

.....HATA UFANYAJE HUWEZI KUWA KAMA MIMI!!!!

Habari yako rafiki yangu!!!
Natumai uko poa sana tu!


 
#....NAKUSHAURI TU KWA ROHO SAFI!!!!
Najua unaweza kufanya vingi sana ambavyo mimi nafanya, ndio tena zaidi hata ya mimi, tena unaweza kupata thawabu sana mbele ya macho ya watu kwa kufanya nifanyayo...ila kwa hakika huwezi kufanya kama mimi kwa kuwa wewe sio mimi na kamwe hautokuwa mimi na hata ukijitahidi namna gani utaishia kuwa wewe mwenyewe!!!


Na jinsi wewe ulivyo ni tofauti na uko  ambavyo hata mimi siwezi kuwa....kama unajaribu kujishindanisha na mimi basi mimi sio kipimio sahihi naam hata mimi kamwe siwezi kushindana na wewe.....kama ingewezekana wewe kufanya kile ninachokifanya basi kusingelikuwa na haja ya mimi kuwepo maana ningekuwepo kufanya nini hali kuna mtu anaweza kufanya kile nilichojia!?
Yamkini hata maamuzi yako mengi ni ya kufuata mkumbo,angalia kwanza wewe ni nani? una nini? na unatamani kufika wapi? na hapo ndio uanze kukazana kuyafikia malengo yako na sio vinginevyo!

Wengi wana dhana vichwani mwao,wanadhani kuna kuwa hai na baadae kuanza maisha...sikiliza hayo uliyonayo ndio maisha....ukisubiri kuishi kesho basi ujue utaishi peponi!!!


Na wengine wanaishi kwa woga sana,wanaogopa watu wanawaonaje au watasemaje na yamkini huumia kwanini hawana pesa au chakula....sikiliza huna haja ya kuogopa!!

WEWE ACHA MAISHA YA MAIGIZO,VAA UHUSIKA HALISI KISHA JIAMINI KATIKA HARAKATI ZAKO UONE KAMA TOFAUTI HAIONEKANI!!!
 
Utaanza kufanikiwa kama ukiwa halisi na ukiamua kuishi maisha yako,naam wewe wa wakati ujao ndio unapaswa kuwa mshindani wa wewe wa sasa....hakuna siku utaanza kuishi....ISHI SASA!!!


UKIACHA KUISHI KAMA WEWE NA KUANZA KUISHI KAMA YULE NA YULE NA IKIWA NA YULE ANAISHI KAMA YULE MWINGINE BASI WEWE NDIO KILAZA WA WOTE KWA IGIZO HILO.....Sasa hao wanaotaka kujifunza kwako wataona nini kwenye nafasi yako?


.......BE YOURSELF!!!!
+255 713 883 797
King Chavala-MC
Twitter @kingchavala
Facebook@King Chavala MC