Tuesday, December 24, 2013

MERRY CHRISTMAS AND HAPPY NEW YEAR!!!

NINAWATAKIENI BARAKA NYINGI ZA MUNGU WAKATI HUU WA SIKUKUU YA NOELI YA 2013 PAMOJA NA SHAMRASHAMRA ZOTE ZA KUUKARIBISHA 2014!!

NINYI NDIO WATU WANGU WA UKWELI , NINYI NDIO MNANIFANYA NIWE NA UJASIRI NA NGUVU YA KUENDELEA KUFANYA NINACHOFANYA!!

SIKUKUU HII IWE  SABABU YA WEWE KUONYESHA UPENDO WA KRISTO KWA WALE WASIOKUWA NACHO!!

SHEREKEA NOELI HII KWA KUWAONYESHA WATU NI JINSI GANI MUNGU ALIVYO PAMOJA NAO!!!

KING CHAVALA MC
+255 713 883 797

Monday, December 9, 2013

KIING CHAVALA na FAMILIA WAFANYA VEMA KATIKA KICHEKO CHA AGANO JIPYA.....Matukio katika picha !!!

KING CHAVALA-MC

The King Of Stand Up Comedy Africa

King Chavala n Richard Chidundo
 JUMAPILI YA TAR 8,DEC 2013 MUNGU ALITUPA KIBALI CHA KUFANYA TAMASHA KUBWA LA UCHESHI WA KIKRISTO LILILOITWA....LAUGH AGAIN CONCERT....Kicheko Cha Agano Jipya!! Heb 8:8-13
PAMOJA NA CHANGAMOTO NA BARAKA YA MVUA KUBWA SANA BADO TULIPATA NAFASI NZURI SANA YA KUCHEKA NA KUCHEKA TENA KATIKA BWANA.....NDANI YA HEMA LA VICTORY CHRISTIAN CENTRE TABERNACLE,DSM TAMASHA LILIFANYIKA LIKIWASHIRIKISHA TAFES DSM PRAISE AND WORSHIP TEAM, ANGEL BENARD, DSM CASFETA PRAISE TEAM, GOD'S GENERATION AND 1ST Q DANCERS...CHINI YA MC GERALD MREMA......JUKWAANI WALIPANDA SAM STAN(UP COMING), RICHARD CHIDUNDO PAMOJA NA MFALME NA MWASISI WA CHRISTIAN STAND COMEDY MWENYEWE,KING CHAVALA-MC!
Tumeitwa kukufurahishwa!!

COMRADE RICHARD CHIDUNDO-MC

"CHACHI" WITH OUR BEST FRIEND PROSPER MWAKITALIMA

 TAFES DSM PRAISE AND WORSHIP TEAM WAS ON BOARD TO LEAD US IN PRAISING AND WORSHIPING OUR GOD!!
SAM STAN....The New Up Coming Stand Up Comedy in LACS Family

God's Generation Dancers wakiwa jukwaani!

 Yoyoyoooo....!!!
 ....UKIVAA SUTI HUWEZI KUCHEZA NAMNA HII!!

ANGEL BENARD AKIIMBA TAMASHANI

MAMA MARY WA YESU AKISHUHUDIA UZURI WA CHRISTIAN COMEDY

OBEID WA THE VOICE AKINENA JAMBO!!

1ST Q DANCERS WAKIWA JUKWAANI

 KING CHAVALA AKIINGIA JUKWAANI TAYARI KWA PRESENTATION!!

RICHARD "CHIDUNDO"&KING "CHAVALA"....<CHACHI>

THE KING OF STAND UP COMEDY AFRICA ON STAGE!!


 YAANI NI FULL SHANGWE....FULL CELEBRATION.....FULL KICHEKO NDANI YA LACS!!
 NA KEKI HII MAALUM NI KWA AJILI YA WATU WOTE LEO.....AHSANTENI KWA KUWA NASI MIAKA 2 SASA NA NDIO MSIMU WA PILI HUOOOO!!
 MAGANIKO WA VUVUZELA AKIPOKEA KEKI USIKU WA KICHEKO CHA AGANO JIPYA!!
KING CHAVALA NA MAMA MARY WA YESU

 NANI ANAWEZA KUCHEZA KIDOGO......
"CHACHI" PAMOJA NA GOD'S GENERATION DANCERS

 "CHACHI" TUKIWA NA CHIEF ACCOUNTANT WETU!!
"CHACHI" PAMOJA NA WAPIGA PICHA WETU

 ...SHORT INTERVIEW AFTER THE CONCERT!!
KING CHAVALA BEFORE THE CAMERA
KWA NIABA YA FAMILIA NZIMA YA LACS, TUNAPENDA KUWASHUKURU WOTE MLIOSAIDIA KUFANIKISHA TAMASHA HILI KWA NAMNA YEYOTE ILE, KIPEKEE NINAWASHUKURU GREAT POTENTIALS LTD,AVANT LTD,MANCON E.A LTD, MITAMBO SOLUTION LTD,SIBUKA TV&RADIO,SHALOM PROMOTIONS,PHOTOGRAPHY EXTREMIST, YOUTH KINGDOM MINISTRIES AND ALL SUPPORTING INDIVIDUALS!!

MUNGU AWABARIKINI SANA MLIPOTOA NA TUNAPOENDELEA KUKUA TAFADHALI MSIKAE MBALI ILI MJIVUNIE MAFANIKIO YETU PAMOJA!!

TUNAWATAKIA KILA LAKHERI NA MUNGU AWABARIKINI SANA!!!

LACS.....Laugh, Relax and Release Yourself!!!

Hotline +255 713 883 797

Wednesday, December 4, 2013

LAUGH AGAIN CONCERT....Kicheko Cha Agano Jipya!!!Chavala Ideas Platform
inakuletea
Tamasha kubwa la kipekee la CHRISTIAN STAND UP COMEDY la kufungia mwaka na kufungua msimu mpya wa mfululizo uitwao LAUGH AGAIN CONCERT SERIES (LACS)
JPILI YA TAREHE 08/12/2013 KUANZIA SAA TISA ALASIRI
ndani ya Hema ya Kisasa ya VICTORY CHRISTIAN CENTRE TABERNACLE (VCCT), MBEZI BEACH A, mwai kibaki rd,kilimani close.
TAMASHA HILI LITAWASHIRIKISHA WACHEKESHAJI KAMA VILE RICHARD CHIDUNDO na wengine kadhaa wanaochipukia,pia 1st Q Dancers and God's generation Dancers bila kuwasahau Ardhi Tafes,DSM Tafes,Casfeta Dsm pamoja na wengineo wengi mmoja mmoja!

Tukatacheka na kusifu sana, tutakata keki na kutoa shukrani kwa Mungu kusaidia kuinua huduma!!

Pia kutakua na Photo both maaluma kwa ajili ya picha!!

Kwa kiingilio 5000/= tu utacheka na kucheka tena na kwa wale wasiopafamu usafiri utakuwepo mwenge kwenda na kurudi saa nane na nusu!!

0713993797
kingchavala.blogspot.com

Monday, November 4, 2013

IJUMAA HII NITAKUWA MOSHI-KILIMANJARO KWA AJILI YA KUSHEREHESHA "BOTTLE PARTY"!!

NI VEMA NUGU KUKAA PAMOJA NA KWA UMOJA,TENA NI VIZURI SANA WATU KUFAHAMIANA KWA KARIBU....KWA NEEMA YA MUNGU IJUMAA HII NITAKUWA MOSHI KWA AJILI YA KUSHEREHESHA USIKU WA KIPEKEE WA KUJUMUIKA KATIKA NA KUFANYA MENGI PAle MANA TABERNACLE NA PIA UTAKUWA NI WAKATI MUAFAKA KUWAKARIBISHA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA!!!
WACHAGA NAJA UPESI!!!

Tuesday, October 29, 2013

HAPPY BIRTHDAY MR ERASTO N.CHAVALA (THE FATHER OF THE KING CHAVALA)!!!

King Chavala-MC & His Lovely Dady
##@ HaPpY BiRthYdAy MR.ERASTO N.CHAVALA (King Chavala-Senior)@#
(**^^My Only and Lovely Biological Dady Au (Baba kwa msisitizo) i have hapa duniani!!!! Leo On 30th October!**@)))

Kuna jumapili moja hivi nilisema sana kuhusu MY Mama na nikaahidi kusema kuhusu Baba!

Mr.ERASTO NATHANAEL CHAVALA ni mtoto wa kwanza kati ya Watoto 11 wa MR.NATHANAEL CHAVALA kama vile mama alivyo lango kwao, Miaka 8 kabla Tanganyika haijapata Uhuru alishakuwepo duniani na Mungu alimsaidia kuwa na akili sana,namaanisha akili sana kwa wakati wake,na hivyo alibahatika kusoma vilivyo kabla Shetani hajamsumbua akikaribia kufanya mtihani wa kidato cha sita,PCB ambapo aliumwa ugonjwa usioeleweka wa tumbo kujaa maji na kuvimba kwa takribani miezi 3 na akapona wakati imebaki wiki kadhaa kufanya mitihani ya mwisho (Inasemekana kuna watu walikuwa wakimchezea na hawakupenda kusoma kwake),basi alimaliza shule na matokeo yake hayakuwa mazuri sana kwasababu hiyo niliyoisema!

Alibahatika kujiunga na Jeshi kama ilivyokuwa ada kipindi hicho, na kwasababu ya upekee wake walimsihi azingatie kuajiriwa na jeshi lakini aligoma maana alikuwa na ndoto zake.
KUNA WAKATI ALIWAHI KATA KABISA TAMAA YA MAISHA NA KUAMUA KUWA MLEVI SANA HUKU AKIWA ANATEMBELEA PIKIPIKI....ILIWAHI KUTOKEA SIKU MOJA ALIPATA AJALI PALE DARAJANI RUAHA-IRINGA NA AKABAKI AKINING'INIA, KIASI AMBACHO ILIKUWA ATANGULIE NA PIKIPIKI IMFUATE JUU NA AFE KABISA....NA HAPO WALITOKEA WASAMARIA WEMA KUMUOKOA,BADALA YA KUSHUKURU ALILAMIKA SANA NA KUFOKA...ETI KWANINI WAMEMUOKOA NA YEYE ALITAMANI AFE TU....MUNGU ni mwaminifu sana maana kila alipojaribu kujiua ilishindikana kwasababu ALIKUWA NA MAKUSUDI NA YEYE, NA MUNGU KWA HAKIKA ALIJUA "The King Of Stand Up Comedy,A Star of Africa" atatoka viunoni mwake!!!
....hapo baadae baada ya kujitambua tena alijiunga na Chuo Cha Kilimo, Uyole Mbeya, na wakati huo kilikuwa Chuo kweli kweli!! na baada ya kuhitimu alipangiwa Ileje na huko akawa AFISA KILIMO WA WILAYA YA ILEJE....Na kwa kipindi hicho alikuwa mtu mkali sana kwa wakulima wazembe na hali hiyo ilisababisha HALI YA KILIMO NA MASHAMBA KUWA SAFI WAKATI WOTE na hivyo maendeleo kukua sana...alifahamika kwa jina la "MUSUMULINGONDO"...Ingawa watu wengi walikuwa wakimwita MSILINGONDO!!....na huku ndiko alikutana na Mama akiwa anafanya kazi katika Hospitali ya Misheni-Kafule kama Mtaalamu wa Maabara (Kazi anayoifanya mama yangu hata leo)
Kwasababu alikuwa wakuja wengi walikuwa wakimuona kama sio mtu wa kawaida na kuna incidence moja imewahi kutokea, ambapo Baba yangu amewahi kupoteza Pochi(Wallet) ikiwa na mshahara wake wote na akatangaza sana wala asijitokeze mtu,kumbe ilikuwa imeokotwa na Mzee mmoja ambaye alikuwa anaogopwa mjini kwa Uchawi....basi siku ulitokea msiba na watu wakajumuika,pamoja na Baba yangu,na wakiwa pale msibani alimuona mtu anatoa pochi na akaitambua kuwa ni ya kwake...basi baba akamfuata na kumuuliza,yule mzee akaakubali kuwa kweli aliiokota na pesa alishazitumia na tangazo alilisikia....hivyo baba akabaki kujua ni kwanini ameona vitambulisho na amesikia tangazo la upotevu na akakaa nayo kimya...akabaki akiduwaa tu....MZEE HUYO ALIKUWA AKIJIAMINI SANA KWA KUWA ALIKUWA ANAOGOPWA MNO!!!...Na wakati wa mazungumzo hayo chakula kilikuwa tayari na Baba yangu aliombwa aondoke pale akale na wenzake(KWANINI?) huyo mzee huwa anakulaga peke yake....Baba akagoma na akasema nitakuwa hapahapa na huyu mzee,basi chakula kikaletwa na akaanza kula,huko mgongoni yakaanza maneno ya hofu, wakimuhofia MSILINGONDO kuwa yamkini nduio ikawa mwisho wa maisha yake...baada ya msiba hata haukupita muda mrefu,wakati watu wanamuhofia Baba yangu,yule mzee alifariki ghafla tu nyumbani kwake....sasa hapo ndio hadithi ikageuka,YAANI KAMA MSILINGONGO AMEMMALIZA YULE MZEE ALIYEOGOPWA BASI HUYO MSILINGONDO NDIO KIBOKO YAO!!!Basi mama hakuishi kwa raha hata kidogo,Baba aliomba uhamisho serikalini akanyimwa,akaomba tena na tena na aliponyimwa kabisa akaamua kuacha kazi na kuamua kuhama kutoka Ileje na kuja Mbozi na Maisha hapo yakaanza upya na amejenga hapo na anaishi hapo hata leo!!

Baba yangu amechangia sana UTU NA HEKIMA nilivyo navyo, ninampenda kwasababu alimpenda sana Mama pamoja na maneno ya mashangazi ya kuudhi bado aliambatana nae kwasababu alijua thamani ya Mama yangu,Baba yangu amewahi kuhukumiwa kufungwa jela mwaka mzima kwa kosa la kugonga mtu na kuua bila kukusudia na wakati huo mama yangu alikuwa mjamzito....ninampenda Baba yangu kwasababu sijawahi kumuona hata siku moja akibishana ama kuzozana au kupigana na mama,kwakweli sijawahi(Yaani hata kama kuna misundestandings huishia chumbani).....Ninampenda Baba kwasababu ananipenda na amefanya kila awezalo kuhakikisha mimi ninakuwa hivi nilivyo sasa!!

BAADHI YA MAMBO AMBAYO BABA YANGU AMENIACHIA,HATA SASA ANGALI YUPO NI HAYA;
1.Kwa baba kusoma ni lazima sio ombi,hata kusoma kuhusu Mungu na kanisa haikuwa ombi,kula wala kuoga sio hiari yako ni lazima!! (BIDII NA KUYAFANYA MAMBO YA MUHIMU KWANZA)
2.Baba hatoi pesa yoyote bila mchanganuo unaoeleweka, kwahiyo unaweza pata pesa yoyote ile uitakayo ikiwa tu unaweza kuitolea mchanganuo wake (ACCOUNTABILITY)
3.Baba akisema jambo amelisema na akirudia ujue kuna adhabu juu yake....na hakuna kazi utakayoifanya bila reward...yaani hata mtihani wa shule kuna zawadi ya ukiwa kati ya 1-3 na kuna zawadi ukifeli!
4.Baba hachapi kwa hasira na hachapi kabla ya mazungumzo na maelewano....yaani ukifanya kosa ni mpaka mjadiliane na wewe ujue kweli hili kosa na mkubaliane adhabu (NEGOTIATION) NA hata ukishaadhibiwa hakuruhusu uondoke machoni kwake!
5.Baba hajawahi kuni-mislead kwenye maamuzi yangu na hata kama ukitaka ushauri lazima akupe option uchague wewe,ingawa nilipomaliza Form6 Tanga Tech alitaka kunishawishi kwa nguvu kusomea Ualimu kwasabau ya Uchumi lakini niligoma na here i am,living and doing what i love most!!!
6.Kila siku tukiwa pamoja Baba alikuwa na jambo la kusema la kutujenga,kwa mfano alikuwa akisimulia hadithi,siku nyingine alisoma neno,siku nyingine alitufundisha nyimbo na siku nyingine alituletea filamu tuone...baba alinitembeza kwenye mashamba na kunionyesha mipaka na kila maamuzi makubwa ndani ya familia hajafanya bila kutushirikisha!!
7.Baba yangu amenisaidia sana sana kumpenda Mungu na kuwa na msimamo wenye nidhamu maishani,amenisaidia sana kuwa makini na maisha,kuelewa tafasiri nzuri ya maisha na kujua umuhimu wa kuwasaidia wengine,zaidi amenifundisha sana KWA KUMPENDA MKE WAKE SANA!!!

SIKU KWETU WOTE TUNAPENDA STORI NA KUCHEKA SANA,YAANI TUKIONANA HUWA TUNACHEKA MNO....NAJIVUNIA BABA YANGU, NINAMPENDA SANA....NIMETAMANI LEO NISEME KIDOGO KUHUSU BABA HUYU,KABLA SIJAANDIKA KITABU KUHUSU FAMILIA YANGU!!
IKIWA LEO NI SIKU YAKO MUHIMU YA KUZALIWA (BIRTH ANNIVERSARY), NATAKA ULIMWENGU WOTE UJUE KUWA BABA NINAKUPENDA SANA SANA, NA NINAKUTAKIA MAISHA MAKAMILIFU....NATAMANI UONE MKE NA WATOTO WANGU NA DAIMA SITAACHA KUJIVUNIA WEWE MAISHANI MWANGU!!!

KAMA WEWE NI RAFIKI YANGU NA UNANIKUBALI SANA ,BASI UJUE HUYU NDIYE MHIMILI WA HIVI NILIVYO,SO USIACHE KUFANYA JAMBO KWA AJILI YAKE....Unaweza kumuombea,unaweza kumsalimia,unaweza kumtumia text,vocha au hata pesa na ukiwa karibu na Mbeya unaweza kwenda kumsalimia.....HAPO ZIMEJAA HEKIMA NYINGI SANA!!!
Mwambieni akiwa hai, mpeni salamu za pongezi, mtumieni furaha za mioyo yenu pamoja nami......hii ni no. ya Baba yangu, naamini itatumika kwa heshima na sio karaha wala ujinga

< 0715 470 526>

Ninawapongezeni nyote mnao-share birthdate na Baba yangu, hongereni pia sana, ninawajua wachache Jesus Up RaphaEl Angela,Ernest Kangajaka,Yulia Raymond,Faraji Nuru, Caroline Mwaipungu,Zaituni Siula na wengineo!!
SALAMU HIZI ZIJULIKANE KWA Hilda Chavala jamii hii yote!!!

THAT IS MY DADY, AND TODAY IS HIS HAPPY BIRTHDAY....I REAL ADMIRE AND LOVE HIM SO MUCH!!!!

Fredy E.Chavala!
+255 713 883 797


NIJAPOKUWA KIMYA....NIPO TIGHT NAFUKUNYUA YALE MAFUKUNYUKU YA CHINI KABISA!!!!

 HABARI ZENU NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI WOOTE TANZANIA,AFRIKA NA DUNIA NZIMA,MIMI NIKO POA NA MZIMA SANA....HAPO KATIKATI NILIKUWA KIMYA SANA NA HAPA SIKUONEKANA KWASABABU NILIKUWA CHIMBO NA NIMEPATA BAHATI YA KUTEMBEA KIDOGO....NIMEKUWA NA WAKATI WA KUTOSHA HYDOM,NIKAWA NA TIME PANDE ZA NAIRODI,NIKAENDA MPAKA KAMPALA,NIKARUDI NAIROBI TENA,KABLA YA KUWA NA MIZUNGUKO MINGI SANA NDANI NYA NCHI!!!
 NIMEKUWA DODOMA MARA NYINGI SANA KIKAZI NA KIHUDUMA,NIMEBAHATIKA KUFIKA IRINGA NA HATA SASA NAREJEA DODOMA TENA KABLA SIJARUDI DAR KWA AJILI YA SAFARI ZA KASKAZINI!!!
 MWEZI WA KUMI NA MOJA NITAKUWA MOSHI NA ARUSHA ALMOST KILA WEEKEND NA MWISHONI NITAREJEA DAR,AHSANTENI SANA WANDUGU KWA KUKUBALI KUTUMIKA NA KUFANYA KAZI NA MIMI!!!
NINAWASHUKURU SANA FASTJET,PRECION AIR NA TROPICAL NA WENGINEO AMBAO NDIO TUNAANZA URAFIKI KWA SASA....KILIMANJARO PIA!!!
BADO TUKO PAMOJA SANA NA DECEMBER 8 TUTACHEKA TENA NDANI YA  HEMA DAR KWA UTUKUFU WA MUNGU NA HILI NI TAMASHA LA KWANZA NDANI YA AGANO JIPYA!!!

NINAWAPENDA SANA
KING CHAVALA-MC
+255 713 883 797

Monday, September 30, 2013

HaPpY BirThDay MC PiLipiLi!!!

LEO TAR 01ST OCTOBER 2013!!
NI SIKU MAALUM KWA KIJANA WETU EMMANUEL MATHIAS-MC PILIPILI, KWANI ANASHEREKEA KUMBUKUMBUKU YAKE YA KUZALIWA MIAKA KADHAA ILIYOPITA...JAPO SIO MINGI KIVIILE!TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUMWEKA HAI NA MZIMA WA AFYA,LAKINI PIA HATUSITI KUTAMBUA KUWA SIKU ZAKE KATIKA HISTORIA ZINAONGEZEKA NA KUFIKIA MWISHO ZINAPUNGUA!

KIJANA HUYU MACHACHARI ALIYEACHANA NA KAZI YA UALIMU NA KUAMUA KUISHI KWA KIPAJI CHAKE,YAANI U-MC NA UCHEKESHAJI,JINA LAKE LIMEENDELEA KUKUA NA KUONGEZEKA KILA LEO,BASI NASI HATUNA BUDI KUFURAHI PAMOJA NAYE KATIKA SIKU HII NZURI,HALI BINAFSI AKIHESABU MAFANIKIO SAWASAWA NA MALENGO YAKE ALIYOKUWA AMEJIWEKEA KUFIKIA LEO!!

NI MUHIMU SANA KWA KUZINGATIA HEKIMA HIZI TATU MAALUM;

1.“Today you are You, that is truer than true. There is no one alive who is Youer than You.”

Theodor Seuss Geisel (1904-1991);
Writer, Cartoonist, Animator

2.“There is neither happiness nor unhappiness in this world; there is merely the comparison of one state to the other. Only a man who has felt ultimate despair is capable of feeling ultimate bliss.”

Alexandre Dumas (1802-1870);
Writer, Author.

3.“Self-acceptance comes from meeting life's challenges vigorously. Don't numb yourself to your trials and difficulties, nor build mental walls to exclude pain from your life. You will find peace not by trying to escape your problems, but by confronting them courageously. You will find peace not in denial, but in victory.”

Swami Sivananda (1887-1963);
Spiritual Leader, Author, Physician

HAPPY BIRTHDAY MY DEAR FRIEND!!


MUNGU AKUPE MACHO UONE YALE YOTE YAKUPASAYO KUONA NA KUYAFIKIA KWA UTUKUFU WA MUNGU!
USIJARIBU KUISHI KWA KUSHINDANA NA YEYOTE WALA KUISHI KUTAKA KUMPENDEZA YEYOTE BALI ISHI KUSUDI LAKO UKIMPENDEZA MUNGU!
MUNGU AKUTANE NA HAJA ZA MOYO WAKO,HATA ZILE AMBAZO HUJAMWAMBIA YEYOTE!


NIKUTAKIE MAISHA MEMA,MAREFU YENYE HESHIMA KWA MUNGU!!

NAKUPENDA!

By kINg cHAaVala (MC) 
+255 713 883797

JOHN LISU KUREKODI DVD YAKE LIVE TAR 06/10/2013

UKO HAPA DVD LIVE RECORDING
 NA JOHN LISSU,
06/10/2013,CCC-UPANGA, DAR ES SALAAM, TANZANIA.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA WOTE;
SALAM TANZANIA!

Shalom Dar es salaam, Shalom Tanzania!
Ndugu wanahabari na watanzania wote kwa ujumla!
Naamini tuko salama na tunaendelea na shughuli zetu za kila siku alizotupatia Mungu wa mbinguni, tumshukuru Mungu sana kwa Amani na utulivu aliotupa na tuendelee kumuomba ili atuepushe na kila aina ya dhahama na uharibifu wa Yule adui!
Kama tulivyosikia hivi karibuni, yale yaliyotokea nchi jirani ya Kenya, kwa hakika tunawapa pole sana kwa mkasa huo, pole kwa wale waliowapoteza wapendwa wao na wale waliojeruhika tunawaombea wapone haraka, tunaamini hekima ya Mungu itakuwa juu ya serikali yao kushughulikia jambo hilo kikamilifu.
Tunamshukuru Mungu kwa zawadi ya uhai, hata sasa tunapoende kumalizia robo ya tatu ya mwaka 2013, tumeshuhudia mambo mengi sana mwaka huu ya kila aina, yapo yale yalionza kwa mara ya kwanza na mengine yamekuwa ni mwendelezo tu wa yale yadumuyo au yalioyaanza hapo kale, tumeshuhudia michezo mbalimbali na vipaji lukuki vikiinuka na kuimarika katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu, na kwa yote mema na mazuri tunampa Mungu Utukufu kwa hakika!


UTANGULIZI JUU YA JOHN LISU;

John Lisu ni mmoja wa waimbaji/Waabudishaji wanaoheshimika katika Tasnia ya muziki wa Injili kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa katika kukuza na kuendeleza muziki wa Injili nchini Tanzania na nje ya Nchi. Nyimbo nyingi alizozitunga na kuziimba zimekuwa zikitumika katika makanisa mbalimbali kama nyimbo za kusifu na kuabudu; pia waimbaji wengine waliokua wakiimba naye wameweza kukua na kufikia uwezo wa kuwa waimbaji wa kujitegemea. John Lisu pia ametia hamasa kubwa miongoni wa wanamuziki wa Injili kuanza kufanya muziki wa live. John Lisu ameweza kufanya tours za ndani ya Tanzania, Africa na Bara la Ulaya kwa ajili ya huduma.
CHRISTINA SHUSHO

John Lisu anategemea kufanya Project II ya Live recoding inayojulikana kama "UKO HAPA" baada ya project ya kwanza ya Jehova yu hai kufanya vizuri sana. Tamasha litafanyika ndani ya ukumbi wa City Christian Centre (CCC) Upanga tarehe 6 Octoba 2013, kuanzia saa 8. mpaka saa 2 usiku.
PAUL CLEMENT

 Tamasha litasindikizwa na waimbaji nguli kama Christina Shusho, Neema Gospel Choir, Paul Clement, Pastor Safari Paul, Bomby Johnson Waimbaji wote wamethibitisha kuwepo. 

BOMBY JOHNSON

VENUE:
City Christian Centre (CCC) mkabala na chuo kikuu cha mzumbe
Si mbali saana kutoka Diamond Jubilee
MIRIUM LUKINDO WA MAUKI


USAFIRI (basi zilizobandikwa matangazo ya tamasha) utakuwepo kutoka posta mpya kwenda ukumbini kuanzia saa saba na nusu mchana kwa bei ya kawaida.
PASTOR SAFARI PAUL

HABARI NJEMA-MUHTSARI!!!!!

Sasa kwa mara pili nchini Tanzania, mwimbaji WA NYIMBO ZA INJILI na mwabuduji JOHN LISSU wa jijini Dar Es Salaam, atakuwa anafanya Ibaada kubwa ama Tamasha la kusifu la Kuabudu(LIVE PERFORMANCE), litakalorekodiwa moja kwa moja (DVD LIVE RECORDING) lenye jina “UKO HAPA” (Yaani Mungu na Uwepo wake).
Tamasha hilo litafanyika jumapili ya Tarehe 6, Octoba 2013  katika Ukumbi mkubwa wa kisasa wa Kanisa la City Christian Centre (CCC)- Upanga, mkabala na Chuo Kikuu Mzumbe – tawi la Dar es salaam, kuanzia saa nane mchana.
Tunataraji watu 5000 kuwa sehemu ya tamasha hili la kipekee,Utakuwa sehemu ya tamasha hilo kwa tiketi ya 10,000/= (kawaida), 20,000/= (VIP) na 3000/= (Watoto);
na Kwale watakaohitaji tisheti maalum za tukio hilo, basi zinapatikana kwa kati ya 12,000-15,000/=, wewe wasiliana tu na (0713905118)
NELLY-MKE WA JOHN LISU


VITUO VYA KUUZIA TIKETI;
1.   MWENGE – Tarakea duka la Kanda
2.   KINONDONI – DPC
3.   MLIMANICITY – Silverspoon Restaurant
4.   KARIAKOO – Mbogo Shop
5.   UKONGA BANANA – KWA GIDO
6.   POSTA - DUKA LA MSAMA

T-SHIRTS

-T-shirts maalumu kwa wanaume na wanawake zinapatikana katika vituo vya kuuzia tiketi kwa bei ya elfu kumi, mpaka elfu 15(kutegmeana na aina).

N.B; Kwa tiketi ya VIP, mnunuzi atajipatia na Audio CD ya John Lissu ya “Uko Hapa”

USAFIRI UTAKUWEPO!!
Siku ya tamasha kutakuwepo usafiri kutoka Posta Mpya mpaka CCC-Upanga,eneo la tukio, hivyo kama wewe ni mgeni na hupafahamu mahali hapo, basi utakachotakiwa kufanya ni kupanda magari toka ulipo mpaka posta mpya kabla ya saa nane,na hapo utayakuta mabasi yenye mabango ya Tamasha, basi utajongea humo na hapo utawezeshwa kufika eneo la tukio, muhimu ni kuzingatia muda!

MUHIMU SANA!!

JOHN LISU NA TIMU NZIMA WAKIWA MAZOEZINI


Tamasha hili ni muhimu sana kwa Tanzania, hasa ukizingatia JOHN LISSU ni mmoja wa waimbaji wa kwanza kuimba live kila mahali anapoalikwa na ni mwimbaji wa kwanza binafsi kufanya LIVE DVD RECORDING pale Ubungo plaza, na ile ya kwanza iliitwa “JEHOVA YU HAI” na sasa anafanya LIVE RECORDING kwa viwango vingine bora zaidi, maana Mungu hutupa hatua moja zaidi kila siku.
Ni muhimu kwa kila mtanzania kujivunia kipaji na tukio hili muhimu katika historia, njoo umwabudu na kumsifu Mungu pamoja, Njoo ujifunze, Njoo umuunge mkono mtanzania mwenzako na njoo uje ufanyike sehemu ya Historia hii kwa Utukufu wa Jehova.
NEEMA GOSPEL CHOIR-KWAYA PEKEE ITAKAYOSHIRIKI "UKO HAPA"


MWALIKO MAALUM;
Kipekee Ninapenda kuwakaribisha wachungaji, mitume, manabii, wainjilisti, waalimu na viongozi wote wa makanisa na huduma mbalimbali, ninawakaribisha viongozi wote wa kisiasa na kijamii kutoka serikalini na vyama vya siasa vyote, ninapenda kuwakaribisha wanaharakati na wanataaluma wote, ninapenda kuwakaribisha waimbaji wote wa nyimbo za injili na wanasanaa wote, ninapenda kuwakaribisa wanafamilia wote, asiwepo wa kubaki nyuma, ninapenda sasa kukukaribisha wewe unaesoma hapa, naam nisaidie kumkaribisha na mwenzako na yeye aje na mwenzake, kimsingi tukio hili ni letu wote bila kujali kitu chochote, njooni tumsifu na kumwabudu Bwana na Mungu hataacha kuibariki Tanzania!
EMMANUEL NDIYE ATAKAYEMPIGIA JOHN LISU LEADING GUITOR


SHUKRANI;
Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Hakneel Production (Wadhamini wakuu), na Jonn Lissu na timu nzima ya maandalizi; Kanisa la CCC-Upanga; vyombo vya habari hususani Praise Power na WAPO Radio; Clouds TV kupitia CHOMOZA na Clouds Radio kupitia GT; Sibuka Tv kupita Gospel Hits; Bloggers hususani Christian Bloggers, magazeti na vyombo vingine vyote vya habari! Shukrani hizi zimfikie kila mtu mmoja mmoja aliyetoa mchango wa mawazo, fedha, ushauri, maombi, ubunifu, yaani mchango wowote wa hali na mali na Mungu awabariki nyote!
MIRIUM LUKINDO WA MAUKI


MUHTASARI MKUU;
Tukio; TAMASHA LA KUSIFU NA KUABUDU, LITAKALOREKODIWA
(DVD LIVE RECORDING CONCERT)
Mhusika; JOHN LISSU
Jina: “UKO HAPA”
Mahali; UKUMBI WA KANISA LA CITY CHRISTIAN CENTRE (CCC)- UPANGA
Lini; 06TH OCTOBA, 2013
Muda; KUANZIA SAA NANE MCHANA
Kiingilio; Tsh 10,000/= (kawaida); 20,000/= (VIP) na 5000/= (Watoto)

Wasindikizaji; CHRISTINA SHUSHO, MIRIUM LUKINDO, PASTOR SAFARI, BOMBY JOHNSON, NEEMA GOSPEL CHOIR-AIC Chang’ombe na PAUL CLEMENT.

Mengineyo; USAFIRI UTAKUWEPO TOKA POSTA MPAKA CCC-UPANGA na Unaweza kujipatia Tisheti pia.
Wahusika; WATU WOTE MNAKARIBISHWA!


UKIPATA HABARI HII USIACHE KUMSHIRIKISHA NA MWENZAKO, NAAMINI HAUTAKOSA TUKIO HILI MUHIMU LA KIHISTORIA KATIKA NCHI YA TANZANIA KWA UTUKUFU WA MUNGU!!

KWA PICHA NA TAARIFA ZAIDI;


http://www.youtube.com/watch?feature=player_detailpage&v=blz0PKQ6QNU
MAWASILIANO:
O713 240 397 – JOHN LISU
0713 905 118 –PROSPER MWAKITALIMA – EVENT MANAGER
0713 883 797 - FREDY CHAVALA - PUBLICITY


Imetolewa na;
Fredy E. Chavala <King Chavala (MC)>
Publicity Manager
+255 713 883 797
On Behalf of The Organizing Committee