LAUGH
AGAIN CONCERT SERIES YA
KING CHAVALA SASA KUJA KIVINGINE 23/09/2012
NDANI YA DPC KINONDONI
BILA KIINGILIO!
....Ni Episode VI ya Season I....LAUGH AGAIN CONCERT.....Revolution!!!
Baada ya Matamasha mengi kufanyika hapa Jijini na lile la
mwisho dogo la washika dau wa karibu kufanyika CCC-Upanga mara ya mwisho,
mwishoni mwa mwezi wa sita, tamasha ambalo liliwakutanisha King Chavala na Gee
and Seth; 1st Q Dancers; J-Sisters;
na Comedians Chidundo na Mrema chini ushereheshaji wa mkongwe Papaa
Sebene-The Blogger sasa The King anakuja na tamasha lingine la kimapinduzi,
moja kutoka mwishoni wa Season ya Kwanza, na mwishoni mwa mwaka wa kwanza wa
LACS na hili ni zawadi ya kipekee kwa wapenzi, washika dau na hata wale washika
hatamu wapya!
Hili Tamasha la Sita la kipekee...na hili litakuwa kubwa
kuliko yote yaliyopita popote, maana baada ya hili kuna lile la mwisho ambalo
litakuwa maalumu kwa ajili ya kurekodi LIVE VIDEO YA COMEDY NA VIPAJI VYOTE VYA
SEASON ONE! Na tamasha la December linakusudiwa kuwa Dec 28,2012 pale
CCC-Upanga.
LAUGH AGAIN CONCERT....Revolution!!!! ni tamasha
la kipekee ambalo halitakuwa na kiingilio mlangoni, ingawa washika dau
wanakaribishwa kuchangia au kuunga mkono kwa namna yeyote ile wanayoweza
kuguswa mioyoni mwenu.....mchango wako unaweza kutufikia kupitia mawasiliano
haya au kwa njia ya benki ya simu kwa no. Hizi (+255 713 883 797 au +255 753
883 797)
LAUGH AGAIN CONCERT.....Revolution!!!
litawahusisha King Chavala pamoja na vijana wake Richard Chidundo na Mc Pilipili...zaidi
kutakuwa na nafasi ya wazi kwa vijana kujaribu kuonyesha vipaji vyao. Zaidi
watu au makundi mengine ambayo yatashiriki ni THE VOICE; GLORIOUS CELEBRATION;
WORDALIVE BAND NA 1ST Q DANCERS na wengine wengi!!
LAUGH AGAIN CONCERT.....Revolution!!!! itafanyika Dar es salaam Pentekoste Church kinondoni(DPC
Kinondoni) tar 23/09/2012 kuanzia
2:30-7:30pm na Hakuna kiingilio,jialike wewe na uwaalike wote!!!
Katika harakati za kukuza vipaji vya kiasili(Natural
talents) na kutambulisha Stand Up Comedy Tanzania; LACS imekuwa ni project ya
kwanza kutembelea mikoa mingi ya Tanzania na kukutana na wadau mbalimbali kama
vile media,makampuni,taasisi,mashirika na makanisa ili tu kwa pamoja wajiunge
katika harakati hizi za kuhakikisha Christian Natural Talents zinapata heshima
ya kutosha na vijana hao wenye vipaji wanachangamkia na kuujenga ufalme wa
Mungu kupitia vipaji hivyo.