Mungu Wangu, Mungu wangu!!
Yaani madamu yametapakaa kila mahali dah!
Hii ni ajali mbaya sana kuwahi kutokea mwaka katika daraja hili aiseee!
Nakwambia ukiona picha huwezi kutamani kabisa kula nyamna!
Tisa wamekufa hapo hapo,tena wanne wamekatika vichwa na watatu wamevunjika miguu yote miwili na hawa wawili ndio Utumbo uko nje kabisa!
Hawa waliobaki hai ni zaidi ya Ishirini na tano lakini hali zao ni mbaya sana na yamkini tukawapoteza wengine ndani ya hizi siku mbili,hapa kila mmoja amechanganyikiwa na wengine wanajizungusha tu hapahapa huku wakilia na hamna wanachosaidia!
Namshangaa sana Mungu maana katika ajali hii kuna huyu mmoja tu, ambaye ni mdogo yeye ndio hajagugwa wala kuchubuliwa hata kidogo.
Naona Watu wengi wanakazana kusaidia kwa juhudi zote,
lakini wengi wanaogopa sana maana hali inatisha na kuna hatari ya wewe unaesaidia kupata majanga pia!
Ahsante Mungu kuna watu wamejiaminisha na hawaogopi hili awala lile na hawa wamesema hata wakiumia au kufa potelea mbali,bora wamejitoa kusaidia pale wanapoweza!
Na kwa mujibu wa Mashuhuda walioshuhudia ajali hii wanasema imesababishwa na mwendokasi wa dereva na ndio maana ikaleta madhara makubwa namna hii!
Yaani ni bonge la hasara,na kama ndio mtu alikuwa anaanza tu kujikwamua,atakuwa ameumia sana nafsini mwake,Jamani msiache kumuombea maana huwezi jua yanayomsibu!
Lakini pia nafikiri kama ile mikanda ingekazwa wala hayo yasingelitokea na inasemekana walijazwa humo kupita kiasi yaani....lakini watu tunakuwa na uchu wa fedha hivyo mpaka tunalazimisha hata idadi ikipitiliza sisi wala hatujali...ona sasa jinsi ajali hii ilivyoleta foleni,yaani magari ya huku hayaendi wala ya kule hayatembei na haijulikani tutavuka saa ngapi hapa!
Kweli
imenisikitisha sana sana maana nasikia vilio tu vya majonzi vya hao
waliobaki na unashindwa ufanye zaidi na wewe unashangaa machozi
yanakutoka tu......Kwa habari zisizo rasmi nimesikia kuwa huyu dereva wa
Lori alikuwa speed sana na aliporuka lile tuta basi tairi la mbele
kulia likapasuka na hivyo likamvuta mpaka akaja akagonga ukingo wa kulia
wa daraja na ndio hapo sasa lile Tenga waliokuwemo hao kuku likaruka
mpaka mbele ya barabara na hivyo msleleko wa Trela ukaja ukapita
katikati ya lile tenga kwa upana na ndio hapo wale kuku tisa wakafa
vibaya palepale kama nilivyowalezea hapo juu....sasa jinsi lile trela
lilivyokaka linaweza kuanguka wakati wowote ule maana linaning'inia juu
ya daraja hivyo wananchi wanaogopa kama wakiingia kuwatoa wale kuku
wazima linaweza kuwakuta la kuwakuta,na kijana mwenyewe inasemekana
mtaji amekopa yaani hapa analia ile mbaya,lakini basi ndio
ishatokea...pole yake kwa kweli...........
Babu: Wewe hebu zima hiyo Tv huoni kama mimi napumzika hapa,au wewe unapenda kusumbua tu watu.
(Babu alipoona huyu mjukuu hasikii akaamka na kumfuata,akamnasa bonge la kibao)
(YAANI BABU TU KUMNASA KIBAO YULE MJUU WAKE)
Akashtuka kumbe alikuwa anaota anaangalia Breeking news ya kwenye TV....Dah ndoto zingine bhana!!
****************************************************
(SAMAHANI JAMANI HIVI SCRIPT YA MOVIE IMEKAA VIZURI? TAFADHALI NAOMBA MAONI YAKO KWA AJILI YA MABORESHO) — in Ruaha, Iringa.