Wednesday, July 3, 2013

.....HATA UFANYAJE HUWEZI KUWA KAMA MIMI!!!!

Habari yako rafiki yangu!!!
Natumai uko poa sana tu!


 
#....NAKUSHAURI TU KWA ROHO SAFI!!!!
Najua unaweza kufanya vingi sana ambavyo mimi nafanya, ndio tena zaidi hata ya mimi, tena unaweza kupata thawabu sana mbele ya macho ya watu kwa kufanya nifanyayo...ila kwa hakika huwezi kufanya kama mimi kwa kuwa wewe sio mimi na kamwe hautokuwa mimi na hata ukijitahidi namna gani utaishia kuwa wewe mwenyewe!!!


Na jinsi wewe ulivyo ni tofauti na uko  ambavyo hata mimi siwezi kuwa....kama unajaribu kujishindanisha na mimi basi mimi sio kipimio sahihi naam hata mimi kamwe siwezi kushindana na wewe.....kama ingewezekana wewe kufanya kile ninachokifanya basi kusingelikuwa na haja ya mimi kuwepo maana ningekuwepo kufanya nini hali kuna mtu anaweza kufanya kile nilichojia!?
Yamkini hata maamuzi yako mengi ni ya kufuata mkumbo,angalia kwanza wewe ni nani? una nini? na unatamani kufika wapi? na hapo ndio uanze kukazana kuyafikia malengo yako na sio vinginevyo!

Wengi wana dhana vichwani mwao,wanadhani kuna kuwa hai na baadae kuanza maisha...sikiliza hayo uliyonayo ndio maisha....ukisubiri kuishi kesho basi ujue utaishi peponi!!!


Na wengine wanaishi kwa woga sana,wanaogopa watu wanawaonaje au watasemaje na yamkini huumia kwanini hawana pesa au chakula....sikiliza huna haja ya kuogopa!!

WEWE ACHA MAISHA YA MAIGIZO,VAA UHUSIKA HALISI KISHA JIAMINI KATIKA HARAKATI ZAKO UONE KAMA TOFAUTI HAIONEKANI!!!
 
Utaanza kufanikiwa kama ukiwa halisi na ukiamua kuishi maisha yako,naam wewe wa wakati ujao ndio unapaswa kuwa mshindani wa wewe wa sasa....hakuna siku utaanza kuishi....ISHI SASA!!!


UKIACHA KUISHI KAMA WEWE NA KUANZA KUISHI KAMA YULE NA YULE NA IKIWA NA YULE ANAISHI KAMA YULE MWINGINE BASI WEWE NDIO KILAZA WA WOTE KWA IGIZO HILO.....Sasa hao wanaotaka kujifunza kwako wataona nini kwenye nafasi yako?


.......BE YOURSELF!!!!
+255 713 883 797
King Chavala-MC
Twitter @kingchavala
Facebook@King Chavala MC

No comments:

Post a Comment