Tuesday, October 29, 2013

HAPPY BIRTHDAY MR ERASTO N.CHAVALA (THE FATHER OF THE KING CHAVALA)!!!

King Chavala-MC & His Lovely Dady
##@ HaPpY BiRthYdAy MR.ERASTO N.CHAVALA (King Chavala-Senior)@#
(**^^My Only and Lovely Biological Dady Au (Baba kwa msisitizo) i have hapa duniani!!!! Leo On 30th October!**@)))

Kuna jumapili moja hivi nilisema sana kuhusu MY Mama na nikaahidi kusema kuhusu Baba!

Mr.ERASTO NATHANAEL CHAVALA ni mtoto wa kwanza kati ya Watoto 11 wa MR.NATHANAEL CHAVALA kama vile mama alivyo lango kwao, Miaka 8 kabla Tanganyika haijapata Uhuru alishakuwepo duniani na Mungu alimsaidia kuwa na akili sana,namaanisha akili sana kwa wakati wake,na hivyo alibahatika kusoma vilivyo kabla Shetani hajamsumbua akikaribia kufanya mtihani wa kidato cha sita,PCB ambapo aliumwa ugonjwa usioeleweka wa tumbo kujaa maji na kuvimba kwa takribani miezi 3 na akapona wakati imebaki wiki kadhaa kufanya mitihani ya mwisho (Inasemekana kuna watu walikuwa wakimchezea na hawakupenda kusoma kwake),basi alimaliza shule na matokeo yake hayakuwa mazuri sana kwasababu hiyo niliyoisema!

Alibahatika kujiunga na Jeshi kama ilivyokuwa ada kipindi hicho, na kwasababu ya upekee wake walimsihi azingatie kuajiriwa na jeshi lakini aligoma maana alikuwa na ndoto zake.
KUNA WAKATI ALIWAHI KATA KABISA TAMAA YA MAISHA NA KUAMUA KUWA MLEVI SANA HUKU AKIWA ANATEMBELEA PIKIPIKI....ILIWAHI KUTOKEA SIKU MOJA ALIPATA AJALI PALE DARAJANI RUAHA-IRINGA NA AKABAKI AKINING'INIA, KIASI AMBACHO ILIKUWA ATANGULIE NA PIKIPIKI IMFUATE JUU NA AFE KABISA....NA HAPO WALITOKEA WASAMARIA WEMA KUMUOKOA,BADALA YA KUSHUKURU ALILAMIKA SANA NA KUFOKA...ETI KWANINI WAMEMUOKOA NA YEYE ALITAMANI AFE TU....MUNGU ni mwaminifu sana maana kila alipojaribu kujiua ilishindikana kwasababu ALIKUWA NA MAKUSUDI NA YEYE, NA MUNGU KWA HAKIKA ALIJUA "The King Of Stand Up Comedy,A Star of Africa" atatoka viunoni mwake!!!
....hapo baadae baada ya kujitambua tena alijiunga na Chuo Cha Kilimo, Uyole Mbeya, na wakati huo kilikuwa Chuo kweli kweli!! na baada ya kuhitimu alipangiwa Ileje na huko akawa AFISA KILIMO WA WILAYA YA ILEJE....Na kwa kipindi hicho alikuwa mtu mkali sana kwa wakulima wazembe na hali hiyo ilisababisha HALI YA KILIMO NA MASHAMBA KUWA SAFI WAKATI WOTE na hivyo maendeleo kukua sana...alifahamika kwa jina la "MUSUMULINGONDO"...Ingawa watu wengi walikuwa wakimwita MSILINGONDO!!....na huku ndiko alikutana na Mama akiwa anafanya kazi katika Hospitali ya Misheni-Kafule kama Mtaalamu wa Maabara (Kazi anayoifanya mama yangu hata leo)
Kwasababu alikuwa wakuja wengi walikuwa wakimuona kama sio mtu wa kawaida na kuna incidence moja imewahi kutokea, ambapo Baba yangu amewahi kupoteza Pochi(Wallet) ikiwa na mshahara wake wote na akatangaza sana wala asijitokeze mtu,kumbe ilikuwa imeokotwa na Mzee mmoja ambaye alikuwa anaogopwa mjini kwa Uchawi....basi siku ulitokea msiba na watu wakajumuika,pamoja na Baba yangu,na wakiwa pale msibani alimuona mtu anatoa pochi na akaitambua kuwa ni ya kwake...basi baba akamfuata na kumuuliza,yule mzee akaakubali kuwa kweli aliiokota na pesa alishazitumia na tangazo alilisikia....hivyo baba akabaki kujua ni kwanini ameona vitambulisho na amesikia tangazo la upotevu na akakaa nayo kimya...akabaki akiduwaa tu....MZEE HUYO ALIKUWA AKIJIAMINI SANA KWA KUWA ALIKUWA ANAOGOPWA MNO!!!...Na wakati wa mazungumzo hayo chakula kilikuwa tayari na Baba yangu aliombwa aondoke pale akale na wenzake(KWANINI?) huyo mzee huwa anakulaga peke yake....Baba akagoma na akasema nitakuwa hapahapa na huyu mzee,basi chakula kikaletwa na akaanza kula,huko mgongoni yakaanza maneno ya hofu, wakimuhofia MSILINGONDO kuwa yamkini nduio ikawa mwisho wa maisha yake...baada ya msiba hata haukupita muda mrefu,wakati watu wanamuhofia Baba yangu,yule mzee alifariki ghafla tu nyumbani kwake....sasa hapo ndio hadithi ikageuka,YAANI KAMA MSILINGONGO AMEMMALIZA YULE MZEE ALIYEOGOPWA BASI HUYO MSILINGONDO NDIO KIBOKO YAO!!!



Basi mama hakuishi kwa raha hata kidogo,Baba aliomba uhamisho serikalini akanyimwa,akaomba tena na tena na aliponyimwa kabisa akaamua kuacha kazi na kuamua kuhama kutoka Ileje na kuja Mbozi na Maisha hapo yakaanza upya na amejenga hapo na anaishi hapo hata leo!!

Baba yangu amechangia sana UTU NA HEKIMA nilivyo navyo, ninampenda kwasababu alimpenda sana Mama pamoja na maneno ya mashangazi ya kuudhi bado aliambatana nae kwasababu alijua thamani ya Mama yangu,Baba yangu amewahi kuhukumiwa kufungwa jela mwaka mzima kwa kosa la kugonga mtu na kuua bila kukusudia na wakati huo mama yangu alikuwa mjamzito....ninampenda Baba yangu kwasababu sijawahi kumuona hata siku moja akibishana ama kuzozana au kupigana na mama,kwakweli sijawahi(Yaani hata kama kuna misundestandings huishia chumbani).....Ninampenda Baba kwasababu ananipenda na amefanya kila awezalo kuhakikisha mimi ninakuwa hivi nilivyo sasa!!

BAADHI YA MAMBO AMBAYO BABA YANGU AMENIACHIA,HATA SASA ANGALI YUPO NI HAYA;
1.Kwa baba kusoma ni lazima sio ombi,hata kusoma kuhusu Mungu na kanisa haikuwa ombi,kula wala kuoga sio hiari yako ni lazima!! (BIDII NA KUYAFANYA MAMBO YA MUHIMU KWANZA)
2.Baba hatoi pesa yoyote bila mchanganuo unaoeleweka, kwahiyo unaweza pata pesa yoyote ile uitakayo ikiwa tu unaweza kuitolea mchanganuo wake (ACCOUNTABILITY)
3.Baba akisema jambo amelisema na akirudia ujue kuna adhabu juu yake....na hakuna kazi utakayoifanya bila reward...yaani hata mtihani wa shule kuna zawadi ya ukiwa kati ya 1-3 na kuna zawadi ukifeli!
4.Baba hachapi kwa hasira na hachapi kabla ya mazungumzo na maelewano....yaani ukifanya kosa ni mpaka mjadiliane na wewe ujue kweli hili kosa na mkubaliane adhabu (NEGOTIATION) NA hata ukishaadhibiwa hakuruhusu uondoke machoni kwake!
5.Baba hajawahi kuni-mislead kwenye maamuzi yangu na hata kama ukitaka ushauri lazima akupe option uchague wewe,ingawa nilipomaliza Form6 Tanga Tech alitaka kunishawishi kwa nguvu kusomea Ualimu kwasabau ya Uchumi lakini niligoma na here i am,living and doing what i love most!!!
6.Kila siku tukiwa pamoja Baba alikuwa na jambo la kusema la kutujenga,kwa mfano alikuwa akisimulia hadithi,siku nyingine alisoma neno,siku nyingine alitufundisha nyimbo na siku nyingine alituletea filamu tuone...baba alinitembeza kwenye mashamba na kunionyesha mipaka na kila maamuzi makubwa ndani ya familia hajafanya bila kutushirikisha!!
7.Baba yangu amenisaidia sana sana kumpenda Mungu na kuwa na msimamo wenye nidhamu maishani,amenisaidia sana kuwa makini na maisha,kuelewa tafasiri nzuri ya maisha na kujua umuhimu wa kuwasaidia wengine,zaidi amenifundisha sana KWA KUMPENDA MKE WAKE SANA!!!

SIKU KWETU WOTE TUNAPENDA STORI NA KUCHEKA SANA,YAANI TUKIONANA HUWA TUNACHEKA MNO....NAJIVUNIA BABA YANGU, NINAMPENDA SANA....NIMETAMANI LEO NISEME KIDOGO KUHUSU BABA HUYU,KABLA SIJAANDIKA KITABU KUHUSU FAMILIA YANGU!!
IKIWA LEO NI SIKU YAKO MUHIMU YA KUZALIWA (BIRTH ANNIVERSARY), NATAKA ULIMWENGU WOTE UJUE KUWA BABA NINAKUPENDA SANA SANA, NA NINAKUTAKIA MAISHA MAKAMILIFU....NATAMANI UONE MKE NA WATOTO WANGU NA DAIMA SITAACHA KUJIVUNIA WEWE MAISHANI MWANGU!!!

KAMA WEWE NI RAFIKI YANGU NA UNANIKUBALI SANA ,BASI UJUE HUYU NDIYE MHIMILI WA HIVI NILIVYO,SO USIACHE KUFANYA JAMBO KWA AJILI YAKE....Unaweza kumuombea,unaweza kumsalimia,unaweza kumtumia text,vocha au hata pesa na ukiwa karibu na Mbeya unaweza kwenda kumsalimia.....HAPO ZIMEJAA HEKIMA NYINGI SANA!!!
Mwambieni akiwa hai, mpeni salamu za pongezi, mtumieni furaha za mioyo yenu pamoja nami......hii ni no. ya Baba yangu, naamini itatumika kwa heshima na sio karaha wala ujinga

< 0715 470 526>

Ninawapongezeni nyote mnao-share birthdate na Baba yangu, hongereni pia sana, ninawajua wachache Jesus Up RaphaEl Angela,Ernest Kangajaka,Yulia Raymond,Faraji Nuru, Caroline Mwaipungu,Zaituni Siula na wengineo!!
SALAMU HIZI ZIJULIKANE KWA Hilda Chavala jamii hii yote!!!

THAT IS MY DADY, AND TODAY IS HIS HAPPY BIRTHDAY....I REAL ADMIRE AND LOVE HIM SO MUCH!!!!

Fredy E.Chavala!
+255 713 883 797


No comments:

Post a Comment