Tuesday, August 26, 2014

MSIONE KIMYA AISEE,NAJIANDAA KUOA MWENZENU 25/10/2014

HABARI ZENU BHANA!!
KWELI NIMEWAMISS MNO MNO, NA MNAWEZA KUWA WENGI MNAJIULIZA MBONA CHAVALA AMEKUWA KIMYA ,NI KWELI YAMKINI,LAKINI MBELE YANGU NINA JAMBO MOJA TU KUBWA ,NALO NI KUOA TAREHE HIYO NIMESEMA ,PANDE ZA MBEYA!!

UKIWA KAMA FAN,RAFIKI AU MTU WA KARIBU SANA, UNAKARIBISHWA SANA KUSHIRIKI TUKIO HILI LA MAISHA KWA NAMNA YEYOTE ILE UNAYOWIWA KUSHIRIKI, IKIWA KWENDA NASI MBEYA BASI NI SAWA ,UKITAKA KUCHANGIA FEDHA,VITU AU MAWAZO NA LABDA ZAWADI,UNARUHUSIWA KUTII UTAYARI WA MOYO WAKO!!

NINAWASHUKURU SANA AMBAO HAWAJAACHA KUTUOMBEA NA KUTUUNGA MKONO IPASAVYO NA IKIWA UNA LOLOTE BASI NI SAWA
0713 883 797(TIGO PESA) AU
0753 883 797(M-PESA)

UNAWEZA NIFUATA FACEBOOK facebook.com/chavalapf

Monday, June 9, 2014

COMING SOON ON 13TH JULY 2014......LAUGH AGAIN CONCERT....Chavala Hatimaye!!!!

 Siku utakayoanza kupambana na Opinions za watu kuhusu wewe na ukasahau kuwa unazo Facts za kutosha kuhusu wewe mwenyewe, hapo ndio utakuwa umeacha kuishi maisha yako halisi na umeanza kuishi maigizo!!

Ukijitambua sawa sawa hutajitahidi kuishi ukiwaonyesha watu jinsi uishivyo ila utajitahidi kumpendeza Mungu na walimwengu sawa sawa na vipimio vya ki-Mungu!! Unapombana na binadamu mwenzio kwa sababu yeyote ile inaonesha kuwa wewe ni MUOGA na unadhani kupambana na wengine ndio kunaweza kukufanya uwe juu, Au huna jambo la maana la kufanya na ndio maana unapata hata muda wa kupambana na wenzio na Au ni Ujinga tu uliochanganyikana na utoto ambao mpaka ukutoke itachukua muda sana!!

Yaani kupigana au kushindana na mwenzio ni sawa na kijiko kiwe na ugomvi na uma au sahani igombane na flampeni kabatini la vyombo hali vyote viko chini ya mwenye nyumba na kila kimoja kimenunuliwa kwa kazi yake na mwenye navyo ndio huamua kipi kifanye nini,kikae wapi na kitupwe lini....sisi sote ni uumbaji wa Mungu,sasa tusemane au kupigana au kushindana ili iweje????/

Nina mengi sana ya kufanya na maisha yangu,yako mengi yananingoja kutimiza na naona muda hata haunitoshi, Ahsante mungu kwa afya njema na akili timamu na msimamo wenye nidhamu katika wewe!







MUHIMU KWA KILA MT:
Tumia muda wako vema na kila siku fanya bidii kutimiza ndoto zako, dini na ujinga havitakufikisha popote, hebu jitafakari tena unatumiaje muda wako!! na ukiona unatumia muda mrefu kufuatilia sijui nani kafanya nini na unatamani kama ungepambana basi ujue una matatizo na ukiendelea hivyo utapotea na kusahaulika kabisa!!!!

Serious people have serious issues to deal with and not other people!!

Think outside the box and be Yourself!!

Tuesday, April 22, 2014

HII NI SERIOUS KABISA, MWAKA HUU KING CHAVALA ANAOA!!

JUMATATU YA JANA NDANI YA HEMA KING CHAVALA AMEWEKA WAZI JINSI ILIVYOKUWA KWAKE CHANGAMOTO KUOA LAKINI HATIMAYE MWAKA HUU ANAOA, AMESEMA TAREHE 20 YA JULY NDIO ATAKUWA ANAMDHIHIRISHA MREMBO HUYO MBELA YA UMMA NA SIKU HIYO HIYO PIA ATAKUWA NA TAMASHA KUBWA KATIKA MFULULIZO WAKE WA MATAMASHA YA COMEDY....LAUGH AGAIN CONCERT....Chavala Hatimaye!!
BASI TUNGOJEE ILI TUJUE YUKO SERIOUS KWELI AU NI COMEDY AS USUAL!!!

Friday, March 14, 2014

LAUGH AGAIN CONCERT....Kicheko Vitani; yafana sana pande za ARUSHA!!!!

King Chavala-MC
 KWA NEEMA ZA MUNGU TUMEFANIKIWA KUANZA RASMI KUFANYA MATAMASHA PANDE ZA ARUSHA NA TAMASHA LETU LA KWANZA TAR 09/03/2014 NDANI YA BETHEL; HAKIKA LILIKUWA ZURI MNO, KATI YA WATU 700-800 WALIHUDHURIA NA KWA KWELI LILIFANIKIWA!
King Chavala; Tolla G na Rafiki mwingine
 TULIKUWA NA WOSHIPPERS; VOT PAMOJA NA ARUSHA MASS KWAYA; KWA HAKIKA MU NGU ALIJITUKUZA MNOOO
Richard Chidundo & King Chavala
 TUKAPIGA PICHA KABLA YA KUANZA TAMASHA NA WATU PIA WAKAPIGA SANA TU YAANI WEWE ACHA TU.....
Adeline pamoja na King Chavala na Richard Chidundo
 VITUKO VYA FURAHA HAVIKUKAUKA KILA KONA....
LACS Team Arusha....Adeline & Huruma
 KWANI WAO NDIO HAWAFAI KUPIGA PICHA??? OKEY KWA HABARI YA MAJIVUNO...HUYO ALISEMA OOOH MIMI MREFU NA HUYU AKASEMA NDIO NA MIMI MNENE.....
Abeignego & Woshippers
 WOSHIPPERS WALIFUNGUA KWA WIMBO MMOJA WA AINA YAKE AISEE,WENYEWE WANAITA OLD SCHOOL HAHAHAH
Ukumbi ukiwa umefurika watu
 NILIFURAHI SANA KUONA WATU WENGI NAMNA HII WAKIFURAHIA TAMASHA MPAKA MWISHO AISEEEE!
Mzee Mbila, mshika dau na mlezi wa King Chavala, Arusha
 KWA MSAADA WA MAWAZO NA MAOM,BIO NA USHAURI WA WATU KAMA HAWA NDIO TUNAZIDI KUSONGA MBELE....
Mama Upendo Mbila, Richard Chidundo, Abeidnego Hango na King Chavala
 YAPENDEZA KAMA NINI NDUGU WAKIKAA KWA PAMOJA NA KWA UMOJA AISEEE...
King Chavala & Upendo Mbilla
 MAMA HUYU NI MKE WA MZEE WA KANISA LAKINI PIA NI MPAMBAJI.MWIMBAJI NA ZAIDI MWANAFUNZI WA OPEN UNI VERSITY....
Shabiki wa Ukweli
 KWA MWENDO HUU LACS IPO MIAKA MIA NANE MBELE,HATA SISI TUKIFA HAHAHAH
Arusha Mass kwaya wakiwajibika vema
 BASI ARUSHA MASS KWAYA NDIO KIBOKO YA SEBENE AISEE...
HApa ni Sebene tu kwa kwenda Mbele
 HIVI UNAWEZAJE KUKAA CHINI WAKATI WENZXAKO WOTE WANANATA NA BITI??
MC Richard Chidundo akiwasilisha jukwaani

WACHEKESHE SANA TU KIJANA....ANASEMA HATA KAMA SURA YAKO NI KAMA MTU MWENYE KICHEFUCHEFU,BADO UMEUMBWA KWA MFANO WA MUNGU.....

 MIMI NA MIONDOKO YAKE TU NABARIKIWA!!!
Mise Anael pia alikuwepo pamoja na Xaxaphone yake aiseee
 KWA KWELI UPENDO NA USHIRIKIANO WA HUYU KAKA HAKIKA UNATIA MOYO SANA SANA, ANAPENDA MNO KUJUMUIKA NASI NA ANATUTIA MOYO SANA....
 King Chavala akijiandaa kuingia jukwaani..je mko tayari????
King Chavala-MC
 .....MFALME CHAVALA YUKO TAYARI KULIVAMIA JUKWAA,KUWASHA MOTO JIONI YA LEO HAHAHAH
King Chavala & Richard Chidundo
 KUNA SAA HUWA TUNAJIKUTA TUNAFANYA PAMOJA KWA STEJI NA HAKIKA HUWA INAPENDEZA KAMA NINI!!
King Chavala on stage making it happen!
 .....NINAPOSEMA KUCHEKA VITANI NINAMAANISHA UNACHEKA KWASABABU UNA HAKIKA NA USHINDI....KWA MFANO VITA YA DAUDI NA GOLIATH WA GATHI UNAICHUKULIAJE?
UKIWAZA SANA UNAWEZA KUSEMA gOLIATH ALIPOOA ALIMVISHA MKEWE PETE KAMA TAIRI LA FUSO HAHAHAH LAKINI DAUDI ALIMTWANGA TU...
Mashabiki na marafiki wakibadilishana mawazo na kupongezana!!
 HAKIKA MAHALI HAPA NI PAZURI....
King Chavala & Dk Arnorld Itemba
NA KWA HAKIKA MOYO UKAFURAHISHWA SANA NA ZAIDI HASA BAADA YA KUONANA NA RAFIKI YANGU NA KAKA YANGU TANGU ENZI TUKO VYUO VIKUU NA SASA HUKU URAIANI,HAKIKA NI MTU MWEMA SANA NA ANANITIA MOYO SANA!!!

BASI BAADA YA HAPO  TUMEMALIZA NA MPAKA HAPO BAADAE TENA!!!

UNA SWALI AU UNATAKA KUJUA LOLOTE ZAIDI, BASI USISITE

+255 713 883 797
lacs.project@gmail.com

Wednesday, February 19, 2014

LAUGH AGAIN CONCERT na KING CHAVALA ndani ya ARUSHA!!!

TAREHE 09/03/2014 NDANI YA UKUMBI WA KANISA LA BETHEL,KIGENGE HAPATATOSHA!!
WAATU WATASIFU NA KUABUDU NA KUCHEKA TENA NA TENA WAKIIFURAHIA INJILI YA BWANA!!
KING CHAVALA PAMOJA UPCOMING COMEDIANS FROM ARUSHA AND DAR,WATAHUDUMU JUKWAA MOJA PAMOJA NA THE VOICE OF TRIUMPH, THE WORSHIPERS, ARUSHA MASS CHOIR, PAMOJA NA FIREPLACE DANCE GROUP!!!
KWA HAKIKA MUNGU LAZIMA ATUKUZWE TU!!!

NI LAUGH AGAIN CONCERT....Kicheko Vitani!!(Season II,Episode II)

HAKUNA KIINGILIO

0713883797/0717567500

Friday, January 31, 2014

NILIJISIKIA VIZURI SANA KUHUDUMU KATIKA USIKU "FRIDAY NIGHT LIVE" NDANI YA CALVARY TEMPLE,ARUSHA!!

 HAPA NDIO MAHALI FRIDAY NIGHT LIVE HUFANYIKA,BWANA ALIWAPA MAONO NAO KWA HAKIKA WAMEYASHIKILIA NA KUYABEBA KWELI,SIACHI KUNYENYEKEA NA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA KUNIONA NAMI KUWA NAWEZA KUHUDUMU KATIKA MADHABAHU HIYO!!


 HII NI SEHEMU YA WATU AMBAO WALIJAA NDANI MPAKA NJE KULIZUNGUKA KANISA USIKU KUCHA!!
 NDANI TUKIENDA SAWA...HUKU NJE PIA KULIKWA NA VYAKULA VYA AINA MBALIMBALI USIKU KUCHA...
 PASTOR PHILIP NAYE ALIKAA HUKU KAMA WAAMUNI WENGINE MARA NYINGI ILI NA YEYE AFAIDI VYA MADHABAHUNI!!
 NELSON NI KIJANA MACHACHARI SANA NA HUYU ANAPIGA MAGITAA,KINANDA PAMOJA NA NGOMA!!
TIMU NZIMA YA KUMBUKUMBU ZA VIDEO NA PICHA MNATO HAWAKUWA NYUMA KUHAKIKISHA KILA KITU KINAREKODIWA IPASAVYO!!!

NA NDIPO ULE WASAA WANGU WA KUHUBIRI KUPITIA COMEDY ULIPOFIKA,NAAM NAMI NILIPOITWA NILIITIKA NA KUKIMBIA MADHABAHUNI,KAMA HAWAKUCHEKA BASI MATESO YAO NI ZAIDI YA MATESO YA MWENYE HAKI,NAAM YAMEZIDI KIPAJI CHANGU!!
 JE UNAWEZA KUMWABUDU BWANA PAMOJA NAMI?.....Yekelekeleeeeee Aaaaahhaaaa......(slow)
 NA MIMI PIA NILIPATA WAKATI WA KUHUDUMU KATIKA MADHABAHU HIYO NA KWA HAKIKA ULIKUWA WAKATI MZURI SANA!!
 THE VOICE OF TRIUMPH NI MOJA YA TIMU AMBAZO ZILIHUDUHU USIKU HUO MAALUM,KWA HAKIKA WALIFANYA VIZURI SANA.....Ninakupendaaaaa Bwanaaaa Bwanaaaaa........
Abeidnego Hango ambaye pia alikuwa mshereheshaji(MC) Usiku huo, pia alipata kuhudumu pamoja na kundi lake linaitwa THE WORSHIPERS!
Nao kwa hakika walifanya vizuri sana.....Amka tumsifu........

USIKU HUO PIA WALIHUDUMU ARUSHA MASS CHOIR,PAMOJA NA KWAYA KADHAA ZA JIJINI ARUSHA NA HAIKUSAHAULIKA KWAYA YA WATOTO WA CALVARY TEMPLE!!


SHUKRANI ZA PEKEE KWA MCHUNGAJI PHILIP,NA WACHUNGAJI WENGINE WOTE PAMOJA NA UONGOZI WA KANISA KWA KUBEBA MAONO HAYA SAWASAWA!!