Friday, January 31, 2014

NILIJISIKIA VIZURI SANA KUHUDUMU KATIKA USIKU "FRIDAY NIGHT LIVE" NDANI YA CALVARY TEMPLE,ARUSHA!!

 HAPA NDIO MAHALI FRIDAY NIGHT LIVE HUFANYIKA,BWANA ALIWAPA MAONO NAO KWA HAKIKA WAMEYASHIKILIA NA KUYABEBA KWELI,SIACHI KUNYENYEKEA NA KUTOA SHUKRANI ZANGU ZA DHATI KWA KUNIONA NAMI KUWA NAWEZA KUHUDUMU KATIKA MADHABAHU HIYO!!


 HII NI SEHEMU YA WATU AMBAO WALIJAA NDANI MPAKA NJE KULIZUNGUKA KANISA USIKU KUCHA!!
 NDANI TUKIENDA SAWA...HUKU NJE PIA KULIKWA NA VYAKULA VYA AINA MBALIMBALI USIKU KUCHA...
 PASTOR PHILIP NAYE ALIKAA HUKU KAMA WAAMUNI WENGINE MARA NYINGI ILI NA YEYE AFAIDI VYA MADHABAHUNI!!
 NELSON NI KIJANA MACHACHARI SANA NA HUYU ANAPIGA MAGITAA,KINANDA PAMOJA NA NGOMA!!
TIMU NZIMA YA KUMBUKUMBU ZA VIDEO NA PICHA MNATO HAWAKUWA NYUMA KUHAKIKISHA KILA KITU KINAREKODIWA IPASAVYO!!!

NA NDIPO ULE WASAA WANGU WA KUHUBIRI KUPITIA COMEDY ULIPOFIKA,NAAM NAMI NILIPOITWA NILIITIKA NA KUKIMBIA MADHABAHUNI,KAMA HAWAKUCHEKA BASI MATESO YAO NI ZAIDI YA MATESO YA MWENYE HAKI,NAAM YAMEZIDI KIPAJI CHANGU!!
 JE UNAWEZA KUMWABUDU BWANA PAMOJA NAMI?.....Yekelekeleeeeee Aaaaahhaaaa......(slow)
 NA MIMI PIA NILIPATA WAKATI WA KUHUDUMU KATIKA MADHABAHU HIYO NA KWA HAKIKA ULIKUWA WAKATI MZURI SANA!!
 THE VOICE OF TRIUMPH NI MOJA YA TIMU AMBAZO ZILIHUDUHU USIKU HUO MAALUM,KWA HAKIKA WALIFANYA VIZURI SANA.....Ninakupendaaaaa Bwanaaaa Bwanaaaaa........
Abeidnego Hango ambaye pia alikuwa mshereheshaji(MC) Usiku huo, pia alipata kuhudumu pamoja na kundi lake linaitwa THE WORSHIPERS!
Nao kwa hakika walifanya vizuri sana.....Amka tumsifu........

USIKU HUO PIA WALIHUDUMU ARUSHA MASS CHOIR,PAMOJA NA KWAYA KADHAA ZA JIJINI ARUSHA NA HAIKUSAHAULIKA KWAYA YA WATOTO WA CALVARY TEMPLE!!


SHUKRANI ZA PEKEE KWA MCHUNGAJI PHILIP,NA WACHUNGAJI WENGINE WOTE PAMOJA NA UONGOZI WA KANISA KWA KUBEBA MAONO HAYA SAWASAWA!!

No comments:

Post a Comment