Thursday, May 17, 2012

MIMI HUWA SIFANYI UCHESHI(COMEDY) WAKATI WOTE!!!....KILA JAMBO LINA WAKATI WAKE!!

(Comedian/Mtumishi/Mjasiriamali thrice in One Chavala)

Shalom my people!
Natumai nyote mu-wazima saana!
Nimetamani sana niseme hili mapema maana kuna watu wengi sana ambao hawanifahamu vema!
Yaani wao kwa kuwa wamesikia mimi ni Comedian basi hudhani kila wakati ni Comedy tu!

(Clown Chavala at Home)

Hapana naomba mjue kuwa I AM VERY SERIOUS PERSON, sema tu wengi hamjapata kunifahamu upande mwingine wa maisha!

Yaani napenda kumtumikia Mungu kwa vipaji na wito huu alioniitia,hivyo saa ya kuomba imetupasa kuomba,saa ya kufundisha imenipasa kufundisha,saa ya kufanya comedy imenipasa hivyo pia na saa ya kutulia kimya imenipasa hivyo!
Mtu yeyote aliye rafiki wa kweli, hutambua haraka sana kuwa leo niko katika hali gani, ila kuna watu kila wanaponiona popote wao hudhani ni muda wa utani kila wakati,lazima mjue kuwa mimi sipendi mizaha
na wala sio mtu wa dhihaka ila comedy ninaifanya kihuduma!
Sio kila kitu kinachoweza kumfanya mtu acheke basi ni comedy hapana,kwa walimwengu hata matusi yanaweza kumfanya mtu acheke,lakini kwangu nitafanya kila niwezalo kukataza,kuonya,kukaripia na kuelekeza njia ipasayo lakini katika hali ya kufurahisha na kupendeza mbele za Mungu!

Natamani Ulimwengu wote unielewe hivyo na kuhusu CHRISTIAN COMEDIES kuna wakati nitaeleza vema inapaswa kuwaje na sio kila ucheshi kwasababu uko kanisani basi uitwe ni christian comedy!!

(Clown Chavala at CCC)

Ahsante mnaonielewa na kuniunga mkono; Bwana atawalipa msipozimia mioyo yenu!!
Mungu awabarikini nyote,Amen!!

No comments:

Post a Comment