Monday, October 15, 2012

CHEKA TENA NA KING CHAVALAHabari yako rafiki!!!
Naamini u mzima wa afya,leo natamani niseme jambo kidogo tu kwa
kuanzia na hii inawahusu watu fulani ambao walikuwa wanapumzika pamoja
ufukweni mwa bahari maeneo ya kigamboni-Dsm!
Basi mmoja alikuwa amekaa akitafakari kwa kina sana huku akiangalia
bahari, mara akaja mwenzake mmoja na kummuliza;
Kijana1: Unawaza nini aisee mbona kama uko mbali sana???
Kijana2: Dah! yaani hapa nawaza kama hii bahari ingekuwa Supu, sijui
ningeweza kuinywa na chapati ngapi!!
Kijana1: Mmmh hahaha wewe ndio sifuri kabisa aisee, yaani unawaza
bahari ingekuwa supu dah!
Kijana2: Sasa wewe unacheka nini? kwani kitu gani cha ajabu hapo?
unajua mimi sipendi dharau!
Kijana1: Aaah acha ujinga wewe, sasa kama bahari hiyo ingekuwa supu
wewe unafikiri moto wa kupikia ungewashwa wapi? na hizo chapati
zingewekwa wapi? hujui kama hizo chapati zingeharibu nyumba za watu
maana zingefunika kila mahali?

Hapo unaweza kudhani labda Kijana1 ana akili sawasawa kumbe mmmh,
maana baada ya muda akasikia yeye akisema
Kijana1: Yaani ningekuwa na pesa, ningenunua bahari yote hii
Kijana2: Hamna kitu wewe,hata kama Biligate angekuwa houseboy wako
huwezi my dear!
Kijana1(akapaniki) kwanini unasema siwezi? kwanini unassiwezi?
Kijana2: Kwasababu mimi siuzi!!

hahahahahaha haya mpaka wakati mwingine Tchaoooo!!!!!

No comments:

Post a Comment