Friday, February 1, 2013

LAUGH AGAIN WITH....KING CHAVALA

ACHENI MADAWA YA KULEVYA,KWELI YANALEVYA ETIIII!!!

Juzi kati nilimkuta teja mmoja mbele ya nyumba fulani kule kinondoni kwa rafiki yangu na huyo Teja alikuwa busy anahangaika kama anatafuta kitu vile,so nikaamua kumsemesha yamkini naweza kumsaidia jambo;
Mimi; Hello Niaje?
Teja; Barida mwana
Mimi; Vipi mwanangu unatafuta nini hapa?
Teja; Mwana nimeangusha ufunguo wa kipadi cha Gheto aiseee,yaani hapa ukamu kishenzi yaani!
Mimi; Kwani Umeangusha hapa? mbona mwanga kibao ingeshaonekana?
Teja; Mmmh nimeangusha kuleeeee(huku akinyosha kidole mbali)
Mimi;Aaah sasa kama umeangusha kule iweje utafute hapa?
Teja; Mwanaaaa kule nilikoangusha nimeona giza kishenzi yaani na sioni kitu,so nimekuja kutafuta hapa maana nimeona hapa kuna mwangaaaaaa
Mimi; Mmmh haya mwanaaaa barida! (IKABIDI NICHEKE KIMOYO MOYO MPAKA NINAONDOKA HAHAHAHAHAH)

...DAH MIMI NILICHOKA KWA KWELI,ILA MADAWA MABAYA,TUACHENI BASI!!!

No comments:

Post a Comment