Saturday, December 1, 2012

HONGERA SANA MR.ELISHA & ORPAH KWA HARUSI NZURI.....By MC CHAVALA!!

Mapambo mazuri ndio ashirio la kwanza la kufana kwa shughuli yoyote ile!!


Nov 4, 2012 ndiyo ilikuwa siku ya kipekee kwa Bwana Elisha kuungana na Bibi Orpah kwa ndoa halali katika kanisa la Kijitonyama KKKT na baadaye kufuatiwa na tafrija ya kufana sana ndani ya ukumbi wa kisasa wa Diomond Jublee Executive...Kwa kweli harusi hii ilifana sana, nimesherehesha harusi na sherehe nyingi sana lakini nina ujasiri wa kusema hii ilikuwa Bab kubwa, kwanza ukumbi ulipendeza mno ndani Orange Colour,viti vya kisasa,vyakula vya kutosha,vinywaji vya kujidai navyo,shampeni kila meza na kilevi hakikurasimishwa katika shughuli hii....Wasimamizi na Maids wote walipendeza mno na kwa kuwa maharusi wote ni waimbaji wa Kwaya ya Uinjilisti kijitonyama KKKT, hivyo kulikuwa na live performance ya timu hiyo...karibu sasa utazame matukio machache kwa faida ya wewe pia kujifunza.

Maharusi wakiingia ukumbini
Hapa ni MC CHAVALA(kushoto) na Hapa set ya Maua ya harusi imekamilika
MC CHAVALA AKIWAMIMINIA SHAMPENI ISIYO KILEVI MAHARUSI
MR.ELISHA & ORPAH WAKIIMBA LIVE PAMOJA NA KWAYA YA UINJILISTI YA KIJITONYAMA(KKKT)
MAHARUSI WAKIKATA KEKI YA KISASA KABISA
Wageni waalikwa wakifuatilia mambo yanavyokwenda

Mh Masilingi(Mb) alikuwa ni mmoja wa wageni maalum wa harusi hii na ndugu wa Bwana harusi
Hongereni sana Elisha na Orpaha kwa hatua hii ya leo

Maharusi wakifurahia chakula cha jioni
NA HIVI NDIVYO HARUSI ILIKUWA INAISHA,AHSANTE SANA BWANA ELISHA NA BI ORPAH PAMOJA NA FAMILIA ZOTE,PAMOJA NA KAMATI YA MAANDALIZI KWA KUNIPA HESHIMA HII KUWA MC WA HARUSI HII,MUNGU AWABARIKI NA NAWATAKIA MAISHA MEMA YA NDOA,AHSANTE!!!


*PICHA HIZI NI KWA HISANI YA
Mana-iPhoto
Dealing with POTRAIT & WEDDING PHOTOGRAPHY
Box 5282 Dsm  Tel: 022 2668562
Cell +255-(754/784/655)-320 955
email; cmgaya2002@hotmail.com

KWA MAHITAJI YA UAANDAJI WA SHUGHULI YA AINA YEYOTE ILE PAMOJA NA MC.MUZIKI ,MAPAMBO NA MENGINE YOTE,TAFADHALI WASILIANA NASI;

MODERN CEREMONERZ
+255 713 883 797
King Chavala(MC)

No comments:

Post a Comment