Thursday, January 10, 2013

POKEENI SHUKRANI ZANGU NINYI NYOTE MLIOIFIKISHA "LAUGH AGAIN CONCERT SERIES" HAPA HUSUSANI MPAKA MWISHO WA Season I(1)

 Habari zenu!
Ninaamini kuwa wote ni wazima na hata walio na madhaifu mbalimbali ya miili,muda sio mrefu mtakuwa sawa,hongereni sana kwa kuingia mwaka mpya wa 2013...HERI YA MWAKA MPYA!!!!
Toka nimeanza kufanya sanaa za jukwaani ni zaidi ya miaka kumi na mbili  sasa,na tangu nimeanza kufanya Comedy na Stand Up Comedy kwa kanisa ni zaidi ya miaka nane,lakini tangu jina limeanza kutajwa tajwa sana ni kama miaka sita hivi na kwa hapa Dar tangu nijitambulishe rasmi kwa sanaa hii ya Stand Up Comedy ni kama miaka mitano sasa,juu ya yote nataka niseme kwamba haijakuwa kazi rahisi hata kidogo kukubalika hususani kwa kile ninachokifanya,ila kwa mara ya kwanza nilipewa kibali cha kupresent kwa hadhira ya watu 12,000 ilikuwa 2009 na ilikuwa njema sana,haikuwa na mashiko saaaana kwasababu ya ukakasi wa watu kutoamini haraka kuwa hii inafaa au laaa,
Juhudi zaidi hazikukoma,nilizidi kufanya,kuelimisha na kufundisha wengine na nilijitahidi sana kuwaelezea watumishi mbalimbali wa Mungu kila tulipokutana,ila bado haikuwa haraka hivyo...wengi walionya kwa ukali,wengine wakanifokea na hata kunisema madhabahuni kuwa watu wasiambatane na mizaha hii kwa kanisa,lakini bado sikukata tamaa kwasababu nilijua for sure watu wataelewa tu siku moja. Kilichonisaidia kiasi fulani ni network ambayo nilikuwa nimejijengea hasa kati ya wanafunzi wa vyuo vikuu ambako mimi pamoja na wenzangu tulikuwa na NGO ambayo kwayo tulifanya Movements za kueleweka na hata sasa bado NGO hiyo ipo na baada ya kuwa kimya kwa muda itarudi tu kwenye mstari,inaitwa HEROES MOVEMENT TANZANIA
Baadae baada ya kufanya na kufanya huku na kule hususani Jijini Dar es Salaam niliazimia kuanzisha project maalum ya matamasha ya Stand Up Comedy na Vipaji halisi....haikuwa kazi ahisi kuanza lakini baada ya.............ITAENDELEA!!!

King Chavala
+255 713 883 797
Facebook; www.facebook.com/chavalapf
Twitter; @kingchavala

No comments:

Post a Comment