Tuesday, February 26, 2013

BIBI KALLOVA AMEPUMZIKA KWA AMANI!!!

NILIPATA TAARIFA ALHAMISI JIONI NA KUSAFIRI IJUMAA USIKU NA KUFIKA IRINGA ASUBUHI YA JMOSI NA MCHANA NIKAAGA NA TUKAMZIKA ALASIRI,NI BIBI YANGU,RAFIKI NA MSHAURI MZURI SANA,HUYU NDIYE MAMA WA BABA YANGU,NDIO ALITESEKA KWA MUDA MREFU PAMOJA NA UZEE BASI IKAWA CHANGAMOTO,AMELALA AMEPUMZIKA KWA AMANI BAADA YA MAISHA YAKE NA MATESO YOTE KIPINDI HIKI CHA MWISHONI,BIBI ALIKUWA MCHAPA KAZI MNO,NA NATAMANI WAKINA NYAMOGA WOTE WAIGE MFANO WAKE,AMEACHA WATOTO 10,WAJUKUU 41 NA VITUKUU 10,NA KATIKA HAO WAJUKUU MIMI NDIO 1ST GRAND SON!!
AHSANTENI WOTE MLIOTUFARIJI NA KUJITOA KWETU TANZANIA NZIMA!!
AHSANTENI REDIO ZA IRINGA NA WANA-IRINGA!
MUNGU AWABARIKINI NYOTE!!

KING CHAVALA
KWA NIABA YA JAMII YA AKINA CHAVALA TANZANIA!!

No comments:

Post a Comment