Sunday, February 17, 2013

'SIWEZI KUWAFANYA MCHEKE IKIWA MIMI SICHEKI MOYONI"-KING CHAVALA

Shalom!
What's up?
Habari yako ndugu yangu,nakuita ndugu yangu kwasababu namaanisha na ninakuona hivyo,kwasababu kama umechukua time yako na kutembelea Blog yangu maana yake umeona kuna jambo la muhimu au nina umuhimu kwako,hata kama sio sana!
Mimi ninamshukuru Mungu sana kwa ajili yako,ninazidi kupiga hatua nyingi zaidi mbele na ninaamini ni kwasababu wewe rafiki na shabiki yangu upo kunitia moyo!
Leo nimetamani niseme jambo hili kwa watu wangu na hii ndio siri ya kipekee iliyojifinya sana!

"SIWEZI KUWAFANYA WATU WACHEKE IKIWA MIMI SICHEKI NDANI YANGU"
Niwapo katika jukwaa la kufanya Stand Up Comedy popote pale kwangu ni madhabahu,ni madhabahu kwasabu mimi sichukulii kama ni burudani tu bali ni mahali pangu pakufikisha habari njema kwa njia ya sanaa hiyo ya ucheshi!
*Inanichukua muda kusoma mambo mengi na kupata muda wa kuyatafakari yale yote ambayo yako katika vipaombele vangu!
HAKUNA NAMNA NAWEZA KUFANYA CHRISTIAN COMEDY BILA KUSIMAMIA MAANDIKO,NA HAUNA NAMNA NAWEZA KUFANYA CHRISTIAN COMEDY AMBAYO MWISHO WA SIKU INALITUKANISHA JINA LA YESU AU KUUDHARAULISHA UKRISTO!!
*Inanichukua muda zaidi wa ku-tengeneza script za skit mpya nilizotunga au ambazo ninazo akiba kuunganisha na maada husika ambayo inahusu mahali nilipo au niliyokusudia moyoni!
*Inanichukua muda wa kutafakari tena kwa upya kwa ujumla,yaani skit-script na muunganiko na maada husika na hapo navaa uhusika wa hadhira na kuona inapokelewaje,na mpaka pale ambapo naona inaleta sense na moyoni ipo amani ya kutosha kuendelea ndipo nasema sasa hii ndio presentation!
*Sasa mwisho sio kwa umuhimu ni kupata muda wa kutosha kuomba special annoint,na hapa ndio ninamshangaa Mungu maana nikiwa katika maombi inaweza ikatokea mpangilio wote wa presentation ukabadilika/ukaboreka au ukabaki uleule lakini wa kufurahisha sana,na hapo ndipo na mimi hucheka sana huku nafsi yangu ikiamanika na kupona ....maana maandiko yanasema Nafsi iliyochangamka ni Dawa! na kwa kuwa Bwana mwenyewe ndio alisema kuwa ataziondoa huzuni zetu na machozi na kutujaza vicheko,basi mpaka pale ninapokuwa nimeaanika moyoni na kucheka sana,ndipo hapo nakuwa niko tayari kuachilia huo upakpo maalumu wa kicheko kwa kila aliyejiandaa kupokea!
Kwa kiingereza wanasema......Releasing the spirit of Laughter/Joy!!
MARA ZOTE HUWA NI MAOMBI YANGU KUWA KILA NIFANYAPO COMEDY POPOTE PALE,BASI ROHO WA BWANA WA UPONYAJI,WA FURAHA,WA KICHEKO NA FURAHA ATEMBEE KWA KILA MTU NA ZAIDI,MUNGU MWENYEWE AHUSIKE KATIKA KUPONYA WAGONJWA,KUWAFUTA WATU MACHOZI YAO NA KUUONDOA UCHUNGU WAO NA ZAIDI KUWAPA UHUISHO MPYA NA WATOKE WAKIWA HAWANA STRESS KABISA!!!

Hivyo nimetamani mjue kuwa ikiwa mimi niko na streess au napita mahali pagumu ambako niko katika utulivu,basi hamna namna naweza kufanya wewe ukacheka,maana ikiwa sina kicheko ndani yangu,je wewe utapata nini?
HIVYO UKIWA MMOJA YA MARAFIKI AU MASHABIKI AMBAO UNGEPENDA HUDUMA YANGU IZIDI KUKUA,BASI USIACHE KUNIOMBEA AMANI NA UTULIVU WA BWANA KILA SIKU,ILI KILA MARA NISIMAMAPO NIWE NACHEKA MOYONI ILI IWE RAHISI KWAKO NA WENGINE WOTE KUPOKEA MGUSO WA KICHEKO TOKA MADHABAHU YA JUU YA MUNGU MWENYEWE!

BY CHAVALA(MC)

No comments:

Post a Comment