Friday, August 2, 2013

CHEKA TENA NA KING CHAVALA.....NGOMA DROO KATI YA BOSI NA HOUSEBOY!!!

HABARI ZENU TENA MARAFIKI ZANGU NYOTE!!
LEO TENA WAKATI NAPANGA NA KUPANGUA MAFILE YANGU NIMEKUTANA NA CLIP HII AMBAYO NILIIFANYA NIKIWA HOME LIKE TWO YEARS BACK!!

NA HII NI HABARI INAYOMHUSISHA BOSSI MMOJA ALIYEKUWA NA MKE NA WATOTO NA PIA ALIKUWA AMEAJIRI WAFANYAKAZI WA NDANI HOUSEBOY(BARAKA) NA HOUSEGIRL(FARAJA);

BOSI ALIKUWA NA TABIA YA KUDOKOA DOKOA NJE YA NDOA NA IKATOKEA AKADOKOA MPAKA HOUSEGIRL, BINTI AMBAYE HOUSEBOY NAYE ALIKUWA AKIMEZEA MATE,NA BAHATI MBAYA YULE BINTI AKAPATA UJAUZITO, MAMA MOJA KWA MOJA AKAMUHISI BARAKA KUHUSIKA LAKINI AKAWA AMEMEZEA KWANZA KUSUBIRI SAA MUAFAKA YA KUMWEKA KITAKO.

YULE BOSI ALIKUWA ANAPENDA SANA WINE, NA BARAKA ALIKUWA NA TABIA YA KUNYWA WINE YA BOSI WAKE BILA KUOMBA NA KILA ALIPOKUWA AKICHUKUA ALIONGEZA MAJI ILI KIMO KIBAKI PALEPALE.

BASI KUNA WAKATI BOSI ALITAFUTA MBINU NA AKABAHATIKA; ALINUNUA WINE AMBAYO AKITIA TU MAJI INABADILIKA RANGI.....BASI BARAKA KAMA ILIVYO ADA AKAJA NA KUMIMINA NA KISHA KUTIA MAJI,SASA ALIPOTIA MAJI TU MARA IKABADILIKA RANGI NA MCHANA HUOHUO BOSI AKAREJEA NYUMBANI NA MKEWE TOKA MATEMBEZINI NA KUKUTA WINE IMEBADILIKA RANGI, BASI YULE BOSI NA MKEWE WAKAKAA SEBULENI NA KUPUMZIKA NA YULE BOSI AKAITA KWA NGUVU BARAKA ALIYEKUWA JIKONI NA MAZUNGUMZO YAO YALIKUWA HIVI;

BOSI; BARAAAAAAKA
BARAKA; NAAM BOSI!
BOSI; NI NANI ALIYEKUNYWA WINE YANGU?
BARAKA; (KIMYA)
BOSI; (AKARUDIA KUITA MPAKA MARA TATU NA KUULIZA)
BARAKA;(NAE AKAITIKA KILA ALIPOITWA ILA HAKUJIBU NENO PALE ALIPOULIZWA)
.....Mara Baraka akakimbia na kuja sebuleni na kusema bosi samahani,yaani ukiwa jikoni,ukiwa umevaa hii na ukiwa unakatakata karoti,husikii kitu chochote isipokuwa jina lako tu ukiitwa,kama huamini na wewe nenda uone
(Basi Mama na Baraka wakamsonga kwa vituko mpaka Bosi nae akavaa epron kwa hasira na kwenda jikoni ili tu athibitishe na akirudi amfute kazi kabisa Baraka)
Basi na Baraka nae akaita....

BARAKA; BOOOOOOSI
BOSI; YES BARAKA!
BARAKA; NI NANI ALIYEMPA UJAUZITO FARAJA?
BOSI;(KIMYA)
BARAKA; (AKAITA TENA NA TENA KWA MBWEMBWE)
BOSI; (NAE AKAITIKA JINA NA KUKAA KIMYA)

Na hapo bosi akarudi kwa kasi sana sebuleni na kusema ni kweli aisee,Baraka nenda kaendelee na kazi tu......Basi akitaka kuondoka akamuuliza mama na wewe unataka kuhakikisha haya

MMMhh MAMA AKASEMA AKHUUU! (Maana anajua mabaya yake yanajulikana na houseboy)

hahahahahaha Cheka na ujifunze!!!

Na King Chavala
MC/Sand Up Comedian
+255 713 883 797

No comments:

Post a Comment