Saturday, August 31, 2013

SALAMU ZANGU ZA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA YA DR. MOSES KULOLA NA KANISA KWA UJUMLA!!!

SHALOM!
NINAJUA KWA HAKIKA MIOYO YENU IMEJAA SIMANZI NA MAJONZI MAKUBWA NA HATA WENGINE HAMUWEZI KUELEZEA,LAKINI NDIO IMESHATOKEA,HATUNA BUDI KUMSHUKURU MUNGU KWA YOTE!

NAOMBA NITUMIE FURSA HII KIBINAFSI KUWAPENI POLE MKE WA MAREHEMU NA WATOTO WOTE WA BABA KULOLA, WA KUZALIWA NA WA KIROHO,PIA NITOE SALAMU ZANGU ZA POLE KWA WAJUKUU NA VITUKUU WOTE!

POKEENI POLE ZANGU KANISA KUPITIA VIONGOZI WOOOTE WA KANISA, NAJUA MKO KATIKA KIPINDI KIGUMU NA NATAMANI MUNGU AWAPE NEEMA,REHEMA NA HEKIMA ILI KAMWE YASITOKEE YAKUTOKEA WAKATI HUU WA MSIBA AU BAADA YA MSIBA,NAAMINI HATMA YA KANISA NI NZURI SANA KAMA MTARUHUSU MUNGU AJITWALIE KIONGOZI WENU MKUU!

NIMEGUSWA SANA NA MSIBA HUU NA MAISHA YAKE YA UTUMISHI,MAOMBI,KUNG'ANG'ANA NA BWANA,IMANI THABITI NA MENGINEYO MENGI AMBAYO HAYATOSHI KUSEMA HAPO,NINASEMA AMENICHANGAMOTISHA NA NATAMANI KUMPENDA YESU SANA SANA NA ZAIDI YA SANA KATIKA MAISHA YANGU!

MZEE KULOLA PAMOJA NA KUWAHI KUPITIA MAKANISA MENGINE BADO HAJAWAHI KUFARAKANA NA WACHUNGAJI WA MADHEHEBU MENGINE YA KIKRISTO,TOFAUTI NA WATUMISHI WETU WA LEO AMBAO WANAGOMBEA WASHIRIKA WALEWALE....NYWELE KUKAKA KICHWANI MIAKA 47,UTUMISHI WA ZAIDI YA MIAKA 60 NA UMRI WA MIAKA 85 NI USHUHUDA TOSHA KUWA MZEE HUYU ALIMAANISHA KUMPENDA NA KUMWAMINI MUNGU!

NA KWA HESHIMA HIYO,NIMEINGIA STUDIO NA KUFANYA NYIMBO 2 KWA AJILI YAKE BABA KU,LOLA, NA HUU UNAWEZA UKAWA KWENYE KOMPYUTA YA KILA MTU ALIYEGUSWA NA MSIBA HUU!


1. MUNGU BABA

2.BABA KULOLA

BASI MUNGU NA AFANYIKE FARAJA YA KIPEKEE KWA KILA MMOJA ALIYEGUSWA KWA NAMNA YA KIPEKEE NA MSIBA HUU!

MUNGU ALITOA NA MUNGU AMETWAA,JINA LA BWANA LIBARIKIWE!!

KING CHAVALA MC
+255 713 883 797

No comments:

Post a Comment