Saturday, August 3, 2013

NINAMSHUKURU MUNGU SANA KWA UPENDELEO ALIONIPA.....JANA NILIKUWA MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI YA CHUO CHA UTABIBU,KIBAHA!!!

HABARI ZENU!
NINAMSHUKURU MUNGU SANA SANA KWA UPENDELEO NILIOUPATA NA ANAOENDELEA KUNIPATIA KILA SIKU.

JAPO NIMEKUWA KIMYA KWA KIASI LAKINI NIMEKUWA NA MAMBO MENGI SANA YANAYOENDELEA CHINICHINI.

NINAMSHUKURU MUNGU TANGU NIMEANZISHA MPANGO MAALUM WA KUWASAIDIA WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI KUJITAMBUA, SASA TUMEFIKA MAHALI FULANI NA TUNAZIDI KUSONGA MBELE,MPAKA SASA NIMESHAFANYA PROGRAM NNE; NA NAAMINI WOTE WALIOFANIKIWA KUHUDHURIA WAMEFAIDIKA SANA NA MAFUNZO YA HUKO.

NA MWEZI WA KUMI NITAZINDUA PROGRAM NYINGINE AMBAYO ITAKUWA INAWAHUSISHA WASICHANA WENYE VIPAJI VYOTE VYA ASILI NA MFULULIZO WA MATAMASHA HAYA UTAITWA "LADIES TALENT BATTLE"...Battling against Evil for the sake of the Kingdom!!....WASICHANA WOTE STAY TUNED!!!

LAKINI PIA NINAMSHUKURU SANA MUNGU KUPATA NAFASI YA KUWASILISHA AU KUSEMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI....KARIBUNI NIMEKUWA ITV, KISHA TBC 1 NA PIA MWANANCHI NA ZAIDI NINACHO KIBALI CHA KUENDELEA KUONEKANA KATIKA VYOMBO VYA HABARI VINGINE.....FURAHA YANGU SIO KUONEKANA TU,BALI NAFURAHI KWASABABU MUNGU AMERUHUSU NISEME, NIFUNDISHE NA KUWAFURAHISHA NA WALE WENGI WALIO MBALI DUNIANI KOTE!

JANA IJUMAA NILIALIKWA KAMA MGENI RASMI KATIKA MAHAFALI YA WANAFUNZI WA UTABIBU WA KIBAHA-COTC (CHUO KIKO NDANI YA HOSPITALI YA TUMBI),WANAFUNZI WALIOSOMA DIPLOMA YAO KWA MIAKA MITATU SASA WANAJIANDAA KUWA MATABIBU HUKO TANZANIA KOTE...HII NI FAMILIA YA TAFES NA KWA HAKIKA SHEREHE HIYO ILIKUWA NZURI SANA!

NILIBAHATIKA KUONANA NA WATU WENGI,WAZAZI WALEZI WA WANAFUNZI HAO NA NAMSHANGAA MUNGU KWA KIBALI NILICHOKIPATA MBELE YA MACHO YAO NA MIOYO YAO!

NA JUMAMOSI MCHANA NITAKUWA SAFARINI KWENDA DODOMA, KESHO NITAKUWA NINAONGEA VIONGOZI VIJANA KATIKA SEMINA YA UONGOZI ILIOANDALIWA NA YKM NA BADO NINAMSHUKURU MUNGU SANA KWA UPENDELEO HUO!!

NATAMANI KATIKA KILA NINALOFANYA JINA LAKE NA YEYE AHESHIMIWE SANA KULIKO KINGINE CHOCHOTE, NAAM NA ANIPE UNYENYEKEVU ILI KAMWE NISIJISIFU WALA KUJIINUA,KWA WALE WALIO ULIMWENGU MWINGINE WATAGUNDUA HII KUWA...UKIWA NA YEYE BASI UNA KILA KITU,AMEN!!

aHSANTENI SANA,MUNGU AWABARIKI,NINAWAPENDA SANA NINYI NYOOOOTE!!
MLIO WA KWELI BASI MSIACHE KUNIOMBEA KILA SIKU!!

Na 
KING CHAVALA
MC/STAND UP COMEDIAN
+255 713 883 797
Facebook; King Chavala MC
Twitter; kingchavala

No comments:

Post a Comment